Kumetokea malumbano makali bungeni nchini Afrika Kusini ambapo wanasiasa wa upinzani wamechelewesha hotuba ya rais Jacob Zuma aliyekuwa akilihutubia taifa na kuzua maswali kuhusu utaratibu.

Julius Malema na wafuasi wake wakitoka bungeni

Baadhi ya wanasiasa wanasema rais huyo hakupaswa kuhutubia bunge kutokana na kashfa mbali mbali alizonazoNi mvutano huo baada ya spika wa bunge la Afrika Kusini mama Baleka Mbete na wafuasi wa upinzani wengi wao kutoka chama cha Ecoomic Freedom Fighters EFF wakiongozwa na Juliasi Malema ambao walikuwa wanadai kutaka utaratibu na kuvuruga hotuba ya Rais Jacob Zuma..
Hatimaye uvumilivu ukamshsinda spika wa bunge Baleka Mbete na kumuru kiongozi wa EFF Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge.
Baada ya fujo hizo Rais Jacob Zuma alijaribu kuendelea kuhutubia lakini wabunge wa upinzani walibaki wakarudia tena kumkatiza

Baada fujo hizo baadae angalau kidogo pakawa na utulivu ambapo Rais Zuma aliweza kumalizia hotuba yake na Katika hotuba hiyo Rais Zuma mbali na mambo mengine alisema serikali yake imekuwa akibana matumizi lakini anaona bado hatua zaidi zinahitajika.

"Tumekuwa tukichukua hatua za kubana matumizi ya fedha za umma kwa hekima ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima. Lakini bila kuathiri wajibu muhimu wa serikali na kutoa huduma kwa raia. Mwaka 2013 waziri wa fedha alitangaza hatua za kubana matumizi. Matumizi ya ziada na yale yasiyo ya lazima yamepunguzwa lakini bado hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kubana upotevu wa fedha za umma."

Rais Zuma anakabiliwa na kashfa kadhaa lakini kubwa la hivi karibuni ni hatua ya kutumia fedha za umma kufanya ukarabati wa kasri lake la kifahari la Nkandla.