Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya jinai (ICC) imetakiwa kushughulikia malalamiko ya Viongozi wa nchi za Afrika wakiishutumu mahakama hiyo kuwa kandamizi kwa nchi za Kiafrika ile hali makosa ya jinai hutokea karibu kila pembe ya dunia.Waziri wa Katiba, Sheria na Haki ,Dr.Harisson Mwakyembe akizungumza katika semina iliyoandaliwa na mahakama hiyo ameitaka kufanyia kazi manung`uniko ya bara la Afrika licha ya Tanzania kuunga mkono shughuli za mahakama hiyo lakini bado iko kwenye msimamo wa nchi hizo.Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Waafrika (PALU) Donald Deya , amesema kuwa mahakama ya ICC inapaswa kujitazama upya na pia viongozi wa Afrika wajitazame pia kwani pande zote mbili zinaonekana kuwa na makosaMahakama ya Kimataifa ya AICC inaendelea na semina ya wiki nzima kwa wanasheria na viongozi mbalimbali juu ya jinsi ya kutumia mahakama hiyo kutetea haki za binadamu na utawala bora.