Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Askofu Gwajima Azushiwa Kifo

  Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, jana alizushiwa kuwa amefariki dunia.

  Taarifa hizo zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia katika hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.  Kwa mujibu wa taarifa hizo zilienea* kuanzia ya saa tano asubuhi, zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia kwa shinikizo la damu.*
  *
  Hata hiyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na mwanasheria wake, wakili wa kujitegemea Peter Kibatala.

  Kibatala jana alisema taarifa hizo ni za uzushi ambao haelewi chanzo chake.

  “Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema Kibata.

  Majira ya jioni jana picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii ziliomwonyesha Askofu Gwajima akiwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: Askofu Gwajima Azushiwa Kifo

  watu hawana nia njema na mchungaji wawa tu
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •