Close

Results 1 to 6 of 6
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

  “Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi.

  Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

  “Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima iyakuwa na mapungufu yake tunacho hitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

  Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

  Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii.

  Na:Mwanahalisonline

  - - - Updated - - -

  Wanaogopa AIBU kama ya jana.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  8
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Re: Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  Yaani katika zama hizi ambazo kuna utitiri wa vyombo vya habari bado kuna wajinga kiasi hiki? Nani kawadanganya kuwa serikali haitaki kuonesha bunge moja kwa moja? Angalia Star TV na Azam TV kupitia channel yake ya Xtra utaona mijadala yote bungeni. Fanyeni utafiti kabla ya kuandika. By the way Rais Magufuli hawezi kuhangaika na hao BAVICHA ambao hata kuchanba hawawezi

 3. #3
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  6
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  Haya matoto majinga kweli sasa nimeamini ule usemi kuwa hadema karibu wote hawana tofauti na nyumbu.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  Quote Originally Posted by Nambalapala View Post
  Yaani katika zama hizi ambazo kuna utitiri wa vyombo vya habari bado kuna wajinga kiasi hiki? Nani kawadanganya kuwa serikali haitaki kuonesha bunge moja kwa moja? Angalia Star TV na Azam TV kupitia channel yake ya Xtra utaona mijadala yote bungeni. Fanyeni utafiti kabla ya kuandika. By the way Rais Magufuli hawezi kuhangaika na hao BAVICHA ambao hata kuchanba hawawezi
  Tatizo hujui tofauti kati ya TBC TAIFA na na hivi vyombo binafsi yaani Star TV na Azam TV.SIJUI NIKUSAIDIEJE.

 5. #5
  Senior Member GURU's Avatar
  Join Date
  Aug 2014
  Location
  Gangstarr
  Posts
  906
  Rep Power
  6
  Likes Received
  26
  Likes Given
  41

  Re: Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  Angalieni Azam TV, ili aiuwe ITV Meziya
  Blade of the Ronin

 6. #6
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

  Quote Originally Posted by Nambalapala View Post
  Yaani katika zama hizi ambazo kuna utitiri wa vyombo vya habari bado kuna wajinga kiasi hiki? Nani kawadanganya kuwa serikali haitaki kuonesha bunge moja kwa moja? Angalia Star TV na Azam TV kupitia channel yake ya Xtra utaona mijadala yote bungeni. Fanyeni utafiti kabla ya kuandika. By the way Rais Magufuli hawezi kuhangaika na hao BAVICHA ambao hata kuchanba hawawezi
  Na wewe uwe unafikilia kabla ya kuandika azam tv inatuhusu nini TBC ni mali ya serikali na inaendeshwa kwa kodi zetu so inapaswa kutoa huduma jamii kama taasisi zengine za serikali

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •