Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Mbunge wa Kilombero Peter Lijuakali Mtata chipukizi katika Anga la siasa kwa sasa

  Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali akitolewa bungeni na polisi.
  DODOMA: KALI ya mwaka. Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali wa Chadema, amechaniwa suti mbili katika matukio mawili tofauti na Jeshi la Polisi ndani ya wiki moja,
  Katika tukio la kwanza, mbunge huyo alitolewa nje kwa nguvu kutoka Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, baada ya kukaidi agizo la mwenyekiti wa kikao, Yahaya Nania la kumtaka asishiriki katika zoezi la kuapishwa kwa madiwani wateule na kumchagua mwenyekiti na makamu wa halmashauri hiyo kwa kili kilichodaiwa kuwa hakuwa mjumbe halali wa baraza hilo.

  Katika purukushani hizo, zilizotokea Januari 24 mwaka huu, ambazo yeye aligoma kutoka akidai ni mwakilishi halali wa wananchi wa jimbo lake, mbunge huyo alichaniwa suti yake katika vuta nikuvute ya polisi.
  Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali


  Katika tukio la pili, Januari 27, mwaka huu, lililosababisha suti yake nyingine kuchanwa na polisi, Lijualikali alikuwa mmoja wa wabunge wa upinzani waliotolewa nje kwa nguvu, baada ya kukaidi amri wa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ya kukaa chini na kutulia.

  Wabunge hao walichukuliwa hatua hiyo baada ya kupinga kujadiliwa kwa hotuba ya rais, aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge Novemba mwaka jana, wakitaka kwanza kupata ufafanuzi wa serikali kwa kitendo chake cha kulizuia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kurusha vipindi vyote vya vikao vya Bunge moja kwa moja (live).

  Kana kwamba haitoshi, wabunge wa upinzani kwa mara nyingine walitoka nje ya Bunge katika kikao chake cha asubuhi, Alhamisi iliyopita baada ya Naibu Spika, Tulia Akson kukataa kusikiliza mwongozo uliokuwa ukiombwa na wapinzani, baada ya Naibu huyo kuzuia kujibiwa kwa swali la mmoja wao kuhusu elimu ya bure.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  6
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Mbunge wa Kilombero Peter Lijuakali Mtata chipukizi katika Anga la siasa kwa sas

  Wakuu huyu si ndiyo alikuwa jela? Kama sikosei alifungwa kwa ujambazi kama nimekosea mtanisaidia.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  8
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Re: Mbunge wa Kilombero Peter Lijuakali Mtata chipukizi katika Anga la siasa kwa sas

  Mkuu mahakama ya kadhi, wala hujakosea. Ni sahihi kabisa kuwa huyo Lijuakali alifungwa jela kwa kushiriki wizi wa magari kama alivyo Godbless Lema

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •