Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  899
  Rep Power
  6
  Likes Received
  41
  Likes Given
  12

  MTATIRO AMSHUKIA WAZIRI MKUU

  WAZIRI MKUU MAJALIWA AMELIDANGANYA BUNGE?
  Na. Mtatiro J
  Jana nilisikitishwa sana na kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi, Freeman Mbowe kuhusu "UPIGAJI MARUFUKU WA SHUGHULI ZA KISIASA ZA VYAMA".
  Majibu ya PM yalionesha namna anavyojaribu kusema "UONGO" hadharani! Jana alidai kuwa alichokisema sicho kilichotangazwa na Vyombo vya habari na kuwa ati "alikubaliana na madiwani wote wakiwemo wa upinzani wa Halmashauri ya Ruangwa na kwamba tamko lile alilitoa kama Mbunge na siyo Waziri Mkuu"!
  Tangu lini Waziri Mkuu akajivua uwaziri mkuu kwenye matamko yake? Na kama tamko lile alilitoa kama mbunge ni mbunge gani anayo mamlaka ya kufuta mikutano na shughuli za kisiasa za vyama?
  Kwanza, ushahidi wa wazi unaonesha kuwa PM huyu alitangaza kauli ya serikali na kuna video moja "iko kwenye kompyuta yangu nyingine" anasikika akieleza kuwa "tumekubaliana serikalini, kuwa mikutano ya kushukuru itatuvuruga......" (akiwaeleza POLISI wa Ruangwa).
  Pili VIDEO ambayo nimeiambatanisha hapa inapingana na anachokisema (Iangalie na uisikilize)!
  Tatu nimewasiliana na Madiwani wa CUF karibia wote walioko Ruangwa wanasema hakuwahi kukubaliana nao jambo hilo.
  Nne, kila mkoa hivi sasa polisi hawataki kabisa mikutano wala shughuli za vyama, mkakati huo umebuniwa ili CCM itumie asilimia 75 ya wabunge na madiwani wake dhidi ya asilimia 25 ya madiwani na wabunge wa UPINZANI.
  Lakini pia yenyewe itaendelea kuwafikia wananchi kwa kupitia "Vyombo vya Serikali" kama vile Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Watendaji wa Kata na Vijiji kuzidi kujiimarisha na kusimamia ajenda zao dhidi ya vyama vya upinzani.
  Kama Waziri Mkuu anajifunza kusema UONGO na PROPAGANDA, Mawaziri wake watajifunza nini kwake? Wakianza kumdanganya yeye kwa mambo ya wazi atasemaje? Hii ni AIBU kama zilivyo aibu nyingine kuu!

  Mtatiro J.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: MTATIRO AMSHUKIA WAZIRI MKUU

  Hata mimi ilinishangaza sana.Sikutegemea waziri Mkuu awe na majibu dhaifu kiasi kile.Kitendo cha kusema kuwa wengine wanaweza kuiga au kuacha kuruhusu mikutano ya siasa kadili wanavyoona inafaa ni ishara tosha kuwa CCM inataka kutumia uwingi wa madiwani wake kuminya Demokrasia.

  Alitakiwa afute kauli yake kwa ustawi wa Demokrasia ya nchi yetu na siyo bla bla.Chama kama ACT-Wazalendo na vyama vingine vichanga vitawezaje kuimarika katika hali hii.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •