Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  8
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Je hoja ya wapinzani ni Bunge kurushwa Live ama mna ugomvi na Nape na TBC?

  Wadau, amani iwe kwenu.

  Nimefuatilia sana mjadala unaoendelea bungeni hususan hoja iliyotolewa na serikali juu ya kutorusha Live baadhi ya mijadala bungeni. Hakika i am totally confused. Ukisikia michango ya wabunge na baadhi ya wadau humu mitandaoni hakika unakuja kugundua kuwa ama hii hoja imepokelewa kisiasa ama kuna watu wameamua kujivika utaahira. Nasema haya kutokana na jinsi michango ya watu ilivyo.

  Ukisikiliza na kuangalia kwa jicho pevu michango hiyo utagundua kuwa kweli tuna safari ndefu. Wapo wanaoamini kuwa Serikali haitaki mikutano ya bunge irushwe live kwa sababu haitaki wananchi waone mijadala inayoendelea bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wapinzani. Wengine wanasema kuwa serikali inataka kuedit kwanza michango ya wabunge ndipo iwafikie wananchi. Wengine wanasema serikali ni waoga sana na hivyo wanaogopa michango ya wapinzani.

  Hakika hoja zote hizi ni za kijinga. Kwa nini nasema hivyo kwa sababu serikali haijapiga marufuku kuoneshwa live kwa vikao vya bunge. TBC1, Star TV na Azam TV wamekuwa wakirusha hewani kipindi cha maswali na majibu bungeni. Then Star TV na Azam TV kupitia Channel ya Xtra wamekuwa wakirusha moja kwa moja mijadala yote inayoendelea bungeni.

  Hakika nimestaajabu sana kuona wabunge wetu wamekuwa wakitoa mapovu kwa mambo yasiyo na tija as if sisi wananchi hatujui nini kinaendelea. Serikali imekuwa very clear kueleza kwa nini wamechukua maamuzi hayo. Hivyo basi wapinzani kuweni wawazi. Msitudanganye sisi wananchi.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Je hoja ya wapinzani ni Bunge kurushwa Live ama mna ugomvi na Nape na TBC?

  LISSU,ZITTO KABWE WAIBWAGA SERIKALI

 3. #3
  Senior Member Tumbo's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Location
  Tanzania
  Posts
  358
  Rep Power
  6
  Likes Received
  18
  Likes Given
  22

  Re: Je hoja ya wapinzani ni Bunge kurushwa Live ama mna ugomvi na Nape na TBC?

  Hii nalo unataka ueleweshwe? Usiwe kama bendera fuata upepo, pia usiwe kama nyumbu wanapotaka kuvuka mto ulojaa mamba, wa mbele akijitoa mwanga na kuamua kupita katikati ya mamba wenye njaa ndani ya mto, haijalishi atavuka Salama ama ataliwa na mamba wote watajirusha mtoni kutaka kuvuka upande wa pili hata kama wataliwa wote, Tbccm ni free air channel kwa kuwa inajiendesha kwa kodi za watanzania wanaotaka kupata habari za Bunge kupitia chombo chao cha umma, hizo zingine huzipati mpaka uwe na king'amuzi chao na uwe umelipia gharama ya kuwa hewani. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
  HAKI ikitendeka, AMANI hutamalaki, hakuna AMANI pasipo HAKI.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Je hoja ya wapinzani ni Bunge kurushwa Live ama mna ugomvi na Nape na TBC?

  Tumbo,huyo hana hata hizo akili za kuambiwa, za kwake atazitoa wapi?.Yupo kwa vile yupo.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •