Close

Results 1 to 3 of 3
Like Tree1Likes
 • 1 Post By Francis Pungumwai

Thread: MUGABE KAITENDEA HAKI TANZANIA; TUITUMIE NAFASI HII VIZURI.

 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  MUGABE KAITENDEA HAKI TANZANIA; TUITUMIE NAFASI HII VIZURI.

  Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ni mfano wa viongozi wa kuigwa kwny suala la uzalendo. Kayika umri wa miaka 92 alionao bado anatambua mchango wa Mwalimu Nyerere na Tanzaia kwa ujumla katika juhudi za ukombozi wa bara la Afrika. Jana amezindua kitabu chake kinachoelezea mchango wa Mwalimu Nyerere katika harakati za ukombozi, kiitwacho "MWALIMU NYERERE; ASANTE SANA"

  Kabla ya kuzindua kitabu hiki Mugabe aliwahi kupingana hadharani na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wanaomtambua Nelson Mandela kama Mkombozi wa Africa. Mugabe aliwaambia Mkombozi wa Afrika ni Nyerere.

  Mwaka 2014 Rais Mugabe aliuambia umoja wa Afrika (AU) kwamba wanapaswa kutambua mchango wa Mwalimu Nyerere na kuuthamini. Alisema inapaswa kuwepo siku maakuu ambayo itaadhimishwa na Afrika nzima kumuenzi Mwalimu Nyerere.

  Gazeti la Daily Nation la tarehe 23 February mwaka 2014 liliandika "Africa should be grateful to Julius Nyerere, says Robert Mugabe"

  Mugabe anasema kumuita Mandela mkombozi wa Afrika ni kupotosha historia. Anasema Mandela alipigania ukombozi wa Afrika kusini peke yake lakini Nyerere alipigania ukombozi wa bara zima la Afrika.

  Baada ya Tanganyika kupata uhuru Nyerere alijikita kusaidia nchi nyingine hususani za kusini mwa Afrika nazo zijipatie uhuru wake. Wanajeshi wa Msumbiji, Zambia, Malawi, Angola, Zimbabwe, Namibia, Botswana, Afrika kusini n.k wameishi maeneo mbalimbali ya Tanzania wakipewa msaada na mafunzo ya kijeshi na jeshi letu la JWTZ.

  Askari wa FRELIMO wasingeweza kuikomboa Msumbiji kama si msaada wa JWTZ. Askari wa Frelimo wamekaa Tanzania hadi wakalowea. Wengine wakaoa dada zetu na wengine wakaacha watoto wao Tanzania. Walipiga kambi maeneo mbalimbali nchini. Pale Iringa kuna eneo hadi leo linaitwa FRELIMO kwa sababu yalikua makazi ya askari hao zamani.

  Si hao tu hata Zambia kina Chiluba, Namibia kina Augustino Netto, Congo ya Patrice Lumumba, Angola ya Dos Santos, Zimbabwe ya Mugabe, Msumbiji ya Samora Machel wote hao ni wanafunzi wa siasa wa Mwalimu Nyerere.

  Hata Afrika kusini yenyewe Mandela ni mwanafunzi wa Nyerere kisiasa. Askari wa ukombozi wa Afrika Kusini wameishi Tanzaia muda mrefu sana na wamepewa msaada mkubwa na watanzania hadi walipofanikiwa kuikomboa nchi yao.

  Joachim Chisano Rais wa zamani wa Msumbiji ameishi Tanzania muda mrefu sana akifanya kazi kwenye mashamba ya mkonge Tanga. Leo ukikutana nae anaongea "kiswahili kilichonyooka" utadhani Mbondei wa "Majani mapana Tanga" kumbe kwake Msumbiji.

  Ikimbukwe pia kuwa Chisano ndiye Rais wa kwanza Afrika kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) kwa Kiswahili mwaka 2001.

  Licha ya Chisano wapo viongozi wengi waliolekewa na kufundishwa uongozi hapa Tanzania. Joseph Kabila amezaliwa hapa Tanzania wakati baba yake akiishi uhamishoni akisaidiwa na JWTZ kuuondoa utawala dhalimu wa Mobutu Sasse Sekko. Kwahiyo Joseph Kabila akazaliwa hapa na kusoma hapa hadi elimu ya sekondari.

  Rais Museveni nae ni zao la Tanzania. Amekulia Tanzania na kusoma chuo kikuu cha Dar Es Salaam na baadae kufundisha chuo cha ushirika Moshi, ambacho kwa sasa kinaitwa Chuo kikuu cha Ushirika.

  Kwahiyo ukimuuliza Museveni anaizungumziaje Tanzania atakuambia "Tanzania ni nyumbani". Maana amesoma hapa na amefanya kazi hapa.

  Msururu wa viongozi wa Afrika waliolelewa Tanzania ni mrefu sana na siwezi kutaja wote nimalize. Lakini pia nchi zilizosaidiwa na Tanzania kujipatia uhuru wake wa kisiasa ni nyingi sana. Ni karibu nchi zote za SADC changanya na za COMESA. Zaidi ya nchi 11 zimesaidiwa na Tanzania kufika hapo zilipofikia.

  Kuna wakati mtu mmoja alisema "Tanzania imekua maskini kwa sababu imesaidia sana nchi nyingi sana". Yani Mwalimu Nyerere hakuwa mbinafsi. Rasilimali kidogo alizokua nazo badala ya kujenga vyuo vikuu vingi, viwanda vingi, barabara, hospitali n.k, yeye akagawa rasilimali hizo. Kidogo tukafaidi sisi na kidogo akazitoa zisaidie wengine.

  Na ukitizama falsafa hii kiundani ina uhalisia fulani. Ukiwa na watu wengi tegemezi huwezi kupata maendeleo ya kiuchumi. Hata kama unalipwa mshahara mzuri kiasi gani lakini unategemewa na wanao, mke, wazazi, wadogo zako, babu, bibi, shangazi, wajomba, watot9 wa shangazi, Mama wadogo, mjomba wa mama yako, baba wakubwa, mashemeji, binamu nk ni ngumu sana kupata mafanikio ya kiuchumi.

  Na ndivyo Tanzania tulivyofanya. Tungeweza kuwa mbali sana kiuchumi lakini ingetusaidia nini kama tungekua nchi tajiri kiuchumi lakini majirani zetu wananyonywa na wakoloni, wanabaguliwa, wananyanyaswa katika nchi yao wenyewe?

  Ndipo Mwalimu Nyerere akaona utajiri katikati ya dhuluma, chuki na unyonyaji wa wakoloni haufai. Bora kutumia rasilimali tulizonazo kusaidia wengine wajikomboe kwanza ndio tufikirie hukusu maendeleo.

  Lajini je hao waliosaidiwa wanakumbuka msaada wetu? Wanathamini? Nadhani hili ndi swali la msingi.

  Ni wachache sana wanaokumbuka na kuthamini. Naweza kusema katika wote angalau Mugabe ameonesha mfano. Nchi nyingine ni ama wametusahau, au wanatupuuza.

  Hawataki kusikia kuhusu Tanzania na ukombozi wala mashuleni hawafundishwi hivyo. Hawataki vizazi vyao vifahamu ukweli huo. Wanataka kubadiki historia.

  Leo ukienda Afrika kusini ukijitambulisha ni mtanzznia watu wa kwanza kukubagua si makaburu, ni raia weusi wa Afrika kusini. Utanzania wako baki nao mwenyewe, hawataki kusikia.

  Nimewahi kwenda mji wa Blantyre nchini Malawi, katika siku kadhaa nilizokaa pale niligundua waMalawi hawaelewi chochote kuhusu Tanzania na hawana mpango wa kuelewa. Zaidi ya Mlima Kilimanjaro hakuna kingine wanajua. Kati ya watu kadhaa nilioongea nao hakuna hata mmoja aliyeweza kumtaja Rais wa Tanzania kwa ufasaha (wakati huo akiwa Kikwete).

  Nikajiuliza mbona sisi tunajua mambo yao? Tunajua viongozi wao?. Tunafuatilia chaguzi zao? Wao mbona hawajishughulishi na mambo yetu? Nikagundua wanatupuuza sana. Wanatuona watu wa hovyo tu na tusio na maana.

  Kipindi fulani pia nilifika Lusaka Zambia. Nikakuta hali kama ya Malawi lakini Wazambia wamezidi. Kwanza wana majivuno ya asili. Wanapenda sifa na kuamini wao ni bora kukiko wengine. Licha ya umaskini mkubwa walionao lakini hawataki kukubali wao ni maskini. Wanaamini Tanzania ni maskini zaidi yao.

  Asilimia kubwa ya mchele unaoliwa Lusaka ni kutoka Mbeya. Wazambia ni wavivu na hawalimi sana japo wana ardhi nzuri. Kwahiyo tunawauzia nafaka kwa kiasi kikubwa lakini bado wanaamini sisi ni maskini zaidi yao.

  Nilikutana na baiskeli nyingi sana za Azam mjini Lusaka, zikiuza "Ice Cream". Nilipowauliza kama wanafahamu ni "product" ya Tanzania walibisha kwa nguvu zote. Wanasema kiwanda cha hizo "Ice Cream" kipo Tanzania lakini mmiliki wake ni "Mzambia" aliyekuja kuwekeza Tanzania. Yani Bakhresa ni Mzambia. Kwa hiyo "product za Azam" ni za Mzambia mwenzao.

  Nikasikitika kidogo lakini moyoni nikasema endeleeni kuamini hivyohivyo kuwa Bakhresa ni ndugu yenu ili azidi kufanya buashara, awauzie hadi "tui la nazi"

  Lakimi nikajifunza kitu kwa hawa jamaa. Hawaamini kama Mtanzania anaweza kuwa na chochote cha msaada kwao. Wanatuona kama "hohehahe" tusio na uelekeo. Ndio maana hata Bakhresa wanasema ni "Mzambia"

  Nilipata fursa ya kuonana na wanafunzi wa chuo kikuu cha Zambia (UNZA) na kupiga nao "story" kidogo. Moja ya mambo yaliyonisikitisha ni wao kuamini eti waliisaidia Tanzania kupata Uhuru. Nikawauliza mmepata uhuru lini? Wakajibu 1964.! Nikawaambia Tanzania tumepata uhuru 1961, sasa hapo nani alimsaidia mwenzake? Wakawa wadogo kama "piriton"

  Ukimuondoa Nyerere ambaye "wanamsikia sikia tu kijuujuu" hawamjui Rais mwingine wa Tanzania. Nikajiuliza mbona sisi tunawajua Marais wao wote toka enzi za Mzee Kaunda, Chiluba, Mwanawasa, Satta na sasa Banda. Nikagundua wanatupuuza sana ndio maana hawana muda wa kujua mambo yetu.

  Makumbusho kuu ya Taifa ya Zambia haina alama yoyote ya Tanzania. Haina hata picha ya Mwalimu Nyerere. Tulipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Tulimuomba afanyie kazi suala hilo. Haiwezekani picha ya Nyerere ikosekane Makumbusho ya Taifa. Mtu aliyewasaidia ukombozi wa taifa lao? Basi watafute hata zile Nyerere alizopiga na mzee Kaunda kama wanaona "wivu" kumuweka Nyerere peke yake.

  Kwa ujumla nimejifunza kuwa nchi zote ambazo tulizisaidia katika Ukombozi hazioni tena umuhimu wetu wala hazikumbuki msaada wetu. Na tusipofanya mkakati wa makusudi historia hii itakuja kufutika. Hali iliyopo Zambia na Malawi ndiyo iliyopo Angola, Namibia, Msumbiji, Congo, Uganda, Afrika Kusini na kwingineko.

  Tunahitaji "mkakati maalumu" wa kutunza historia hii ili hata vizazi vijavyo viweze kuelewa. Hivyo basi nashauri ufanyike mkakati wa makusudi wa serikali Yetu kuongea na serikali za nchi zote tulizozisaidia ili katika mtaala wao wa Elimu waweke somo maalumu la ukombozi wa nchi zao na namna Tanzania ilivyowasaidia.

  Katika kuandika mtaala huo waje wajionee maeneo ya Iringa, Dodoma na Morogoro mahali ambapo tuliwapa hifadhi babu zao wakipigania ukombozi wa nchi zao. Historia hiyo itunzwe vizuri na iwe somo la lazima kwa kila mwanafunzi.

  Hii itasaidia kurudisha hadhi yetu kimataifa na kuweka historia sawa.

  Haya mambo ya kusema "Mandela ni mkombozi wa Afrika" wakati mkombozi sahihi ni Mwalimu Nyerere yanatokana na kutokujua historia. Haya mambo ya mwanafunzi wa chuo kikuu Zambia kuamini kwamba wao waliisaidia Tanzania kupata uhuru ni kutokujua historia.

  Asante Mugabe kwa kuweka historia sawa. Asante kwa kutambua mchango wa mwalimu Nyerere na Tanzania katika ukombozi wa bara la Afrika. Kupitia Mugabe tumepata "point" ya kuanzia. Tutumie fursa hiyo kushawishi nchi nyingine tulizozisaidia katika Ukombozi nazo zifuate nyayo za Mugabe.
  CARLOS.MAJURA likes this.

 2. #2
  Senior Member GURU's Avatar
  Join Date
  Aug 2014
  Location
  Gangstarr
  Posts
  906
  Rep Power
  6
  Likes Received
  26
  Likes Given
  41

  Re: MUGABE KAITENDEA HAKI TANZANIA; TUITUMIE NAFASI HII VIZURI.

  Mugabe kaongea point ni kweli kabisa japokuwa historia za nchi nyingi ni magumashi. wanawatambua watu ambao hawakuwa na mchango wowote na kuwaacha the real warrior.
  Blade of the Ronin

 3. #3
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  6
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: MUGABE KAITENDEA HAKI TANZANIA; TUITUMIE NAFASI HII VIZURI.

  Mugabe yupo sahihi shida ya wanasiasa wengi wanafiki siyo wakweli kama mugabe.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •