Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Wapinzani walivyo watolea uvivu Polisi wakati wakitoka nje ya Bunge

  Baada ya juzi wabunge wa upinzani kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa kichapo kutoka kwa polisi, jana walitoka tena kimya kimya na kuwatolea hasira zao askari waliokuwa nje ya jengo la kutokea ukumbini.

  Tangu asubuhi jana, kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge, kulikuwa na idadi kubwa ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), ambao walikuwa wamevalia mavazi maalumu ya kuzuia risasi.

  Wabunge wa upinzani walipotoka nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya kipindi cha maswali na majibu kwisha, askari hao walisogelea eneo la mlango wa kutoka kwenye ukumbi huo.

  Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wabunge hao kuanza kuwazomea polisi hao na kila mmoja kusema alilojisikia.

  Baadhi ya maneno yaliyokuwa yakitamkwa dhidi ya polisi hao ni pamoja na “leo cheni hamuibi” , ‘ingieni tena leo Bungeni mkachangie na nyie” ‘leo hampati wa kumpiga”, “nendeni mkachangie ndani huko, kikao cha familia kinaendelea”, “leo hamuibi tumewa-time”, “Ingieni ndani kwenye kikao cha NEC kinaendelea huko” “Hebu waangalieni, watoto wa maskini mnakubali kutumiwa”.

  Wengine walikuwa wanasema, “leo mmekuja wapya ili muibe vizuri, hamuambulii kitu, mtaendelea kutumiwa hivyo hivyo".

  Naye Zuberi Kuchauka wa Liwale (CUF), anayedaiwa kupigwa na askari hao juzi na kuachwa na fulana, alikuwa akinyoosha juu kidole chake kilichokuwa kimefungwa kitambaa akidai aliumizwa na askari hao.

  “Nawaambieni hii damu mliyoimwaga mtailipa. leo hamumpigi mtu hapa nawaambia,” alisema.

  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge, Freeman Mbowe, alipozungumza na waandishi wa habari jana, alisema kuna wabunge wa upinzani wamelalamika kwamba wameibiwa vitu mbalimbali vikiwamo mikufu, simu na pochi.
  hakikisha hupitwi na habari

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  536
  Rep Power
  6
  Likes Received
  20
  Likes Given
  1

  Re: Wapinzani walivyo watolea uvivu Polisi wakati wakitoka nje ya Bunge

  ndio serikali ya magufuli serikali ya kihuni na ndungai anaendesha bunge kihuni ndio maana alitaka kumuuwa yule kijana aliyekuwa anagombea huko

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •