Close

Results 1 to 8 of 8
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  8
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Wadau, amani iwe kwenu.

  Taarifa rasmi nilizopata toka kwa mdau wangu muhimu ndani ya CUF ni kwamba chama hicho hakitafanya makosa ya kususia uchaguzi wa Marudio Zanzibar. Kwamba, kwa kufanya hivyo ni kujiondoa moja kwa moja kwenye siasa za Zanzibar na kutoa mwanya kwa hasimu wao, CCM kujinafasi na kujiimarisha zaidi.

  Mdau huyo amenidokeza kuwa tamko lililotolewa na Baraza Kuu ni danganya toto kwa CCM ili wajisahau na kutoweka mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi huo kwa kuamini kuwa watashiriki bila ya mpinzani wao mkuu, CUF. Mdau huyo amesema kuwa CUF wametafakari kwa kina uamuzi wa kujitoa kwenye uchaguzi huo na tamko lililotolewa si uhalisia wa msimamo wa CUF. Kwamba, kwa kuwa hakuna mikutano ya kampeni itakayofanyika, CUF itaendelea na mikakati ya ndani ya kushiriki uchaguzi huo huku kwenye public wakifanya hadaa ili CCM wajisahau.

  Mdau amenidokeza kuwa kwa vile hakuna kampeni zitakazoruhusiwa, CUF imejipanga kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi wa kishindo.

  Wadau, jukumu langu ni kuwahabarisha tu. CCM msilale mlango wazi. CUF wanawavizia ili mkilala fofofo watoke na mwali wenu.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Mnajisumbua bure wala hawana muda huo

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,227
  Rep Power
  8
  Likes Received
  73
  Likes Given
  3

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Niko Zanzibar, hayo uliyoyasema ni mkweli mkuu, kuna watu wanapita kimyakimya kuhamasisha upigaji kura na ni vyama vyote lakini wengi wao ni CUF na CCM. kwa ujumla CCM hapa Visiwani wanajua huo ujanja wa wapinzani wao na kiukweli nao wamejipanga.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Tatizo lenu hamjiamini wao wameshasema hawatoshiliki uchaguzi na taarifa hizo zitafika mpaka tume ya uchaguzi sasa hizo kampeni za chinichini mnazosema nyinyi ni upotoshaji

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2014
  Posts
  802
  Rep Power
  6
  Likes Received
  62
  Likes Given
  126

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Quote Originally Posted by TataMadiba View Post
  Niko Zanzibar, hayo uliyoyasema ni mkweli mkuu, kuna watu wanapita kimyakimya kuhamasisha upigaji kura na ni vyama vyote lakini wengi wao ni CUF na CCM. kwa ujumla CCM hapa Visiwani wanajua huo ujanja wa wapinzani wao na kiukweli nao wamejipanga.
  Uko huko kuiba kura; wala huna haja ya kufanya hivyo maana CUF (machotara wako) wamewatamkia hawashiriki. Hao watakaoshiriki ni sawa na vijana wa masabuli waliojivika uchadema. Hao ni CCM waliojivika uCUF

 6. #6
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  536
  Rep Power
  6
  Likes Received
  20
  Likes Given
  1

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  CUF haiwezi kuingia kwenye uchaguzi wa kihuni kama huo unao andaliwa na ccm

 7. #7
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  8
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  CUF haiwezi kufanya ujinga wa kutoshiriki uchaguzi

 8. #8
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  6
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Tahadhali kwa CCM, Mpinzani wenu CUF atashiriki uchaguzi Zanzibar. Msidanganyike

  Cuf wasiposhiriki uchaguzi tunawazika na habari yao itakuwa ndiyo mwisho kwenye siasa.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •