Najua wapo watakaobeza na kutukana lakini tusema tu ukweli kutokujua KIINGEREZA imesababisha wengi wetu kutokujiamini na kutokujua dunia inaelekea wapi.

Kataa kubali dunia inaendeshwa kwa kujua KIINGEREZA yani kuweza kuelewana na mataifa mengine na hata wewe mwenyewe kujifunza na kuelewa.

Watanzania tumebaki kuiga tu kwa WENZETU yale ambayo hayaitaji kujifunza. Yanapokuja ya kujifunza au hata kuingia kwenye mitandao ili ugoogle kutafuta kitu fulani tunashindwa kwasababu hatujui lugha.

Ivyo wengi wetu wamebaki kuiga wanavyovaa, wanavyoimba Wamarekani,Waingereza kwasababu kuimba au kuvaa hakuitaji kuongea au kusoma.

Inapokuja maswala ya kutaka kujua namna mabunge ya wenzetu linaendeshwaje au kujua kiwanda fulani linazalishaje bidhaa zake hapo tunakuwa sifuri. Tunakuwa waoga kuuliza kwasababu hatujui KIINGEREZA tunakuwa wanyonge.

Kutokujua KIINGEREZA imetufanya watanzania kutokujua dunia inakwenda wapi.
WATANZANIA TUNAJUA TU WIMBO GANI KAIMBA Mmarekani na mchezaji gani wa mpira ni wa Chelsea au Manchester.

NDIO MAANA WATANZANIA VIJANA NA TUNAOWAITA WASOMI WANABURUZWA NA SERIKALI WANVYOTAKA BILA KUPAZA SAUTI ZAO KWASABABU
"HATUJUI DUNIA INAKWENDA WAPI NA TUNATAKA NINI"
tupo tupo tu bora kumekucha. Tunaowaita wasomi ndio balaa hawajui chochote kwasababu wengi wao wanavyeti vya kununua na kukariri, anayo degree lakini uelewa wake sawa na Mtoto aliye darasa la saba.

Tunaibiwa na watendaji wa serikali tuliowaweka sisi na ushahidi upo wazi wazi, hata kama wamesafishwa lakini ni Kashfa tayari yani tuseme "CV IMECHAFUKA" bado tunawakumbatia na kuwasifia na kuendelea kuwaweka kwenye nafasi za juu, nyeti ili watuongoze.

Yanayotokea hapa Tanzania hayawezi kutokea katika nchi ambayo raia wao wanauelewa.