Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, 64, anakaribia kujiuzulu baada ya kukiri kuwa amewaangusha mashabiki (Sun), Van Gaal atakuwa na mazungumzo na makamu mwenyekiti wa United Ed Woodard kujadili jinsi ya kukatisha mkataba wake unaokwenda hadi mwaka 2017 (Star), Woodward amezungumza na wachezaji wakuu wa United kuhusiana na mikakati ya Van Gaal na anafikiria kumteua Ryan Giggs kuwa meneja hadi mwisho wa msimu (Mail),Meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, 52, anazidi kupata matumaini ya kuwa meneja wa Manchester United (Times), meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Manchester United wangekuwa tayari wamempa kazi Jose Morinho, kama wangekuwa wanamtaka, na anadhani wanasubiri hadi mwisho wa msimu kujaribu kumchukua meneja wa Bayern Munich, Pep Guardiola, 45, au Diego Simione, 45 kutoka Atletico Madrid (Telegraph), Liverpool wamekubaliana maslahi binafsi na Shaktar Donetsk, kumsajili mshambuliaji Alex teixeira, 26 (Futbol Ukraine),

Hata hivyo bado hakuna muafaka juu ya ada wanayotaka kutoa Liverpool na bei iliyowekwa kwa mchezaji huyo kutoka Brazil (Liverpool Echo), kiungo wa Fiorentina Mario Suarez anafikiria kuhamia Watford (Mirror), Roma wamethibitisha kuwa wanazungumza na Jiangtsu Suning ya China kuhusiana na kumuuza mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho, 28 (Guardian), mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Greizman, 24, amesema hana mpango wa kuondoka Spain na kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 75 (Telefoot),

Chelsea wamekuwa wakimalizia kukamilisha usajili wa Alexandre Pato, 26, kutoka Corinthians kwa mkopo, huku wakitazamia kumsajili moja kwa moja baadaye (Mail), Newcastle wamepunguza kasi ya kumnyatia winga wa Tottenham Andros Townsend, 24 kutokana na Spurs kutaka pauni milioni 14 (Sky Sports), Newcastle wanaonekana kufanikiwa kubaki na kiungo kutoka Ufaransa, Moussa Sissoko, 26, lakini mchezaji huyo amesema huenda akaondoka mwisho wa msimu (Sun),

mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke, 25, huenda akaondoka Anfield baada ya michuano ya Euro 2016 (Bleacher Report), nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, 29, anakabiliwa na jeraha jingine la msuli wa mguu na huenda asicheze kwa mwezi mmoja zaidi (Star). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye magazeti ya leo Ulaya. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Zimesalia siku saba kabla ya dirisha hili la usajili kufungwa. Siku Njema!!