Meya wa Ilala, ni Charles Kuyeko (Chadema) amepata kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) amepata kura 31.

Uchaguzi huo umefanyika kwa madiwani wa Ukawa pekee baada ya madiwani wa CCM kususia uchaguzi huo kwa madai kuwa baadhi ya wajumbe wake kuzuiliwa kupiga kura kutokana na kutokuwa na vigezo.

Baada ya mvutano huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ameamua uchaguzi huo uendelee kwani madiwani wa Ukawa walikuwa wanatimiza kolamu.