Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka akimpongeza Mbwana Samata kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa Afrika, Wakati wa hafla ya kumpongeza iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na wadau wengine wa Soka na kufanyika katika hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka, wakati walipokutana katika hafla ya kumpongeza Mbwana Samata aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika. Kushoto ni Mchezaji bora wa Afrika 2015 Mbwana Samata.Waziri wa Nyumba na Makazi William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Mauzo Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka wakati wa hafla ya kumpongeza Mbwana Samata kwa kutwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa afrika iliyofanyika katika hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara imesema kuwa bado inaufanyia kazi ushauri wa serikali wa kuwa mmoja wa wafadhili wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Mbagala katika kumuenzi mwanasoka wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika.

Wakati wa hafla ya wadau wa soka ya kumpongeza mwanasoka huyo juzi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam,mgeni wa heshima kwenye hafla hiyo Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi,William Lukuvi aliwataka wadau wa kuendeleza soka nchini ikiwemo kampuni ya Vodacom inayofadhili ligi kuu kumuenzi Samatta kwa vitendo kutokana na heshima aliyoiletea Tanzania ikiwemo kujenga uwanja aliokuwa anachezea kabla ya kiwango chake kuwa kikubwa na kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki ligi ya daraja la kwanza.

Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania,Herieth Koka amesema kuwa ushauri huo wa serikali ni mzuri katika kumuenzi mwanasoka Samatta na kampuni ya Vodacom itaufanyia kazi.

Vodacom ikiwa ni mdhamini mkuu wa ligi ya soka nchini tumefurahishwa na mafanikio ya Samatta kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni yetu ni kusaidia michezo hususani mchezo wa soka wa kuwa tunaamini kuwa bado kuna fursa ya vijana wengi wa Tanzania maisha yao kuwa murua kupitia.

Alisema pia kuwa kampuni itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine wa soka nchini kuhakikisha ligi kuu ya Vodacom inazidi kuwa bora ili wapatikane wachezaji wengine wa kuitangaza Tanzania katika ramani ya soka duniani kama alivyofanya Mbwana Samatta.