Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika Pierre-Emerick Aubameyang akishuka kwenye ndege ya Rais wa nchi hiyo mara baada ya kuwasili mjini Libreville, Gabon. Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba alitoa ndege yake ikamchukue Aubameyzng na kumleta nchini Gabon baada ya kutangazwa mshindi. Alipowasili alipokelewa na maelfu ya wananchi na baadae kufuatiwa na hafla fupi aliyoandaliwa Ikulu ya Gabon. Hapa kwetu Tanzania Shujaa wetu Mbwana Samattaambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa ligi za ndani, hajapokelewa hata na Mkuu wa Wilaya. Mbaya zaidi katua usiku wa manane kama "mchawi".. eti TFF wanatoa utetezi dhaifu kuwa CAF walimkatia ticket ya usiku. Yani mwenzenu kapelekewa NDEGE YA RAIS ikamchukue, nyie mnajitetea na ticket ya usiku wa manane ya CAF?? Subhana Allah.!