Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  473
  Rep Power
  5
  Likes Received
  10
  Likes Given
  6

  Warioba kufukuzwa

  WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameandikiwa notisi ya kufukuzwa katika jengo analolitumia kama ofisi ya kuendeshea shughuli za kisheria, Raia Mwema linafahamu.
  Serikali kupitia Wakala wa Majengo (TBA) imeamuandikia notisi hiyo Warioba ikidai kuwa nyumba hiyo inatakiwa na serikali kwa matumizi mengine na kwamba haitaendelea kumpangisha baada ya mwisho wa mwezi huu (Desemba, 2015).
  Nyumba inayozungumzwa hapa ni ile inayotumiwa na kampuni ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu iliyopo katika Mtaa wa Ghuba, namba 501/13 ambayo iko katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa barua yenye Kumb. Na. GC:2/210/043/II/4 iliyoandikwa Novemba 11 mwaka huu, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo ya Serikali, Mhandisi Elius Mwakalinga, amemuandikia Warioba (kupitia kampuni hiyo ya uwakili) notisi hiyo akisema ni matarajio yao kwamba kampuni hiyo itazingatia maelekezo ya wakala.
  “Hii ni kukuarifu kwamba nyumba hii inatakiwa na serikali kwa matumizi mengine hivyo tunakujulisha kuwa baada ya upangaji wako kuisha mwezi Desemba 2015, hatutaendelea na upangishaji wa nyumba hiyo,” aliandika Mwakalinga.
  Alipohojiwa na Raia Mwema kuhusu suala hilo, Warioba alikiri kupokea barua hiyo lakini hakutaka kuingia kwa undani kueleza kuhusu hilo.
  “ Hilo ni tatizo kati ya mwenye nyumba na mpangaji. Kwa sasa, kwa kadri ninavyofahamu, suala hilo liko mahakamani. Sina maelezo marefu zaidi ya hayo,” alieleza Warioba ambaye ni mmoja wa viongozi mashuhuri hapa nchini.
  Hatua hiyo ya TBA kutoa notisi imekuja katika wakati ambapo kesi iliyofunguliwa kuhusu shauri hilo la nyumba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam bado haijatolewa hukumu. Kesi hiyo ni namba 91 iliyofunguliwa mwaka jana.
  Katika kesi hiyo, kampuni hiyo ya Warioba inapinga ongezeko la kodi ya pango iliyofanywa na TBA pasipo kuwashirikisha na pia kupandisha mara tatu ya kiwango kilichokuwa kinalipwa na kampuni hiyo maarufu ya uwakili hapa nchini.
  Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizoko katika maandishi ya upangaji kati ya TBA na kampuni hiyo, Warioba na wenzake walianza kupanga katika nyumba hiyo mwaka 2001; wakiibadilisha nyumba hiyo kutoka katika makazi na kuifanya kuwa ofisi chini ya makubaliano maalumu na wakala.
  Wakati wakianza kupangishwa, kodi katika nyumba hiyo ilikuwa kiasi cha shilingi 150,000 kwa mwezi, kiwango kilichokuwa kimepangwa kwa kuzingatia gharama ambazo kampuni hiyo ya Warioba ilikuwa imeingia kwenye ubadilishaji wa nyumba hiyo kutoka makazi kuwa ofisi.
  Katika kesi ambayo kampuni ya Warioba imefungua Mahakama Kuu, maelezo yanaonyesha kuwa ilitumia kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya matengezo na upanuzi wa jengo hilo.
  Katika kesi hiyo ambayo sasa itachukua sura nyingine baada ya uamuzi huo wa TBA kuandika notisi, kampuni ya Warioba na wenzake inaonyesha kwamba mwaka 2007, kodi katika nyumba hiyo ilipandishwa na kufikia shilingi 700, 000 (laki saba) kwa mwezi kabla ya kupandishwa na kuwa shilingi 900,000 (laki tisa) kwa mwezi, mnamo mwaka 2009.
  Kilichokuja kuharibu uhusiano kati ya pande hizi mbili ilikuwa ni hatua ya TBA kupandisha kodi ya nyumba hiyo kutoka shilingi 900,000 hadi shilingi milioni 3.9 mwaka 2013. Ongezeko hilo ni takribani mara tatu ya kiwango kilichokuwa kinalipwa awali.
  Baada ya juhudi za kujaribu kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo zilishindikana na ndipo kampuni hiyo ya Nyalali, Warioba& Mahalu ikaamua kwenda Mahakama Kuu kutafuta haki.
  Raia Mwema linafahamu kwamba Aprili 04, 2013, TBA ilipeleka barua kwa kampuni ya Warioba kueleza nia yake ya kuongeza kodi kwa kiwango kinachoendana na thamani ya soko pamoja na kuzingatia gharama za utunzaji wa nyumba hiyo.
  Kwa mujibu wa barua yenye Kumb. Na. 2/210/043/75 iliyosainiwa na Mhandisi F.W Tarimo kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TBA, barua hiyo ilieleza kwamba kodi iliyokuwa ikilipwa na kampuni ni kidogo na hivyo inalazimika kuongezwa.
  “Kodi inayotozwa kwa nyumba za maeneo ya jirani na jengo hili ni kati ya dola za Marekani 15 hadi 18 kwa mita ya mraba kwa nyumba za kuishi ambapo kwa ofisi iko juu zaidi ya hapo. Kiwango kilichotumika kwa jengo husika kiko chini zaidi ya kiwango kilichotajwa hapo juu.
  “Tunapenda kukujulisha kuwa mikataba yetu haina kipengele cha kumhusisha mpangaji katika ukadiriaji wa kodi ya pango. Aidha, katika mkataba wako ulioisha imeelezwa kuwa kodi itahuishwa kila baada ya miaka miwili kutokana na kuongezeka kwa gharama mbalimbali za uendeshaji,” ilisema barua hiyo.
  Gazeti hili limefanikiwa kuona nakala ya majibu ya barua hiyo iliyoandikwa na Warioba mwenyewe kwenda kwa Tarimo. Barua hiyo yenye Kum.Na. NW/WJ/O1/13 iliandikwa Aprili 10, 2013 na Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Tanzania alitoa maelezo marefu kuhusu mgogoro wa nyumba hiyo.
  “ Kwanza niseme hatujakataa ongezeko la kodi kwani ilikwishakubalika kwamba kodi ingekuwa inaongezeka kila baada ya miaka miwili. Hilo lilikubalika tangu mwaka 2007.
  “Katika barua yako umesema hakuna kipengele cha kumhusisha mpangaji katika ukadiriaji wa kodi ya pango. Lakini, naamini huo ni utaratibu mzuri wa kusikiliza na pia kuwa wazi (transparent). Kwa msingi huo, naamini ni jambo jema tuendelee kushirikiana,” aliandika Warioba.
  Ni kwenye barua hiyo ya Warioba ndipo aliomba kuwe na mazungumzo baina ya pande hizo mbili kuhusu namna ya kutatua mgogoro huo. Hata hivyo, juhudi hizo hazikuzaa matunda na sasa TBA imeamua kumfukuza Jaji Warioba na wenzake katika ofisi hiyo.
  Katika barua ya Novemba 13 mwaka huu kutoka kwa kampuni ya Nyalali, Warioba & Mahalu kwenda TBA ambayo Raia Mwema pia limefanikiwa kuona nakala yake, Warioba anashangazwa na wakala huyo kuandika notisi ya kuwahamisha, wakati suala hilo liko mahakamani.
  “ Kipengele ulichotumia kutuandikia notisi ni cha mkataba ambao hatujakubaliana na ndiyo kiini cha shauri lililo mahakamani. Kutoa notisi ya aina hii ni kudharau Makahama. Msimamo wetu ni kungoja uamuzi wa Mahakama. Kwa misingi ya sheria, notisi yako ni batili,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
  Juhudi za kumpata Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, kueleza kuhusu suala la notisi hiyo kwa Warioba hazikuzaa madai kwa vile alielezwa kuwa likizo na kwamba hatapatikana hadi atakaporejea ofisini Januari 06, mwaka huu

 2. #2
  Senior Member kichondi77's Avatar
  Join Date
  Mar 2014
  Posts
  183
  Rep Power
  6
  Likes Received
  11
  Likes Given
  5
  Dhambi ya usaliti ni mbaya sana
  You can fool some people some time but you can't fool all the people all the time

 3. #3
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: Warioba kufukuzwa

  Wacha wamtoe nishai tu huyu mnafiki, ndiyo maana alitandikwa makofi na makonda.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Warioba kufukuzwa

  Washamtumia.Wa nini tena

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •