Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  473
  Rep Power
  5
  Likes Received
  10
  Likes Given
  6

  Ushahidi dhidi ya Kubenea kuanza kutolewa Jan 20

  Mashahidi sita wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea (44), wataanza kutoa ushahidi wao Januari 20 na 21, 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Kubenea anakabiliwa na kesi ya kumtolea lugha chafu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Desemba 14 eneo la Mabibo External walikokwenda kutatua mgogoro wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd.

  Hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba jana aliyasema hayo baada ya wakili wa Serikali mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kumsomea maelezo ya kesi hiyo mshtakiwa huyo ambayo baadhi aliyakana.

  Akisomewa maelezo hayo na wakili Mutalemwa, mshtakiwa huyo alikiri kuwa ni mbunge wa Ubungo na mlalamikaji katika kesi hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda na Desemba 14,2015 alifika katika Kiwanda hicho kulikokuwa na mgomo wa wafanyakazi.

  Hata hivyo, alipoelezwa kuwa anashtaka kwa kosa la kutoa lugha ya chafu, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo.

  Wakili huyo alidai siku hiyo, mshtakiwa huyo alimtolea lugha chafu Makonda kuwa ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo chake ni cha kupewa.

  Alidai kuwa kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu

 2. #2
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  6
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Ushahidi dhidi ya Kubenea kuanza kutolewa Jan 20

  Kubea anatakiwa afungwe maana hana akili tumecheka na ujinga wake.

 3. #3
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: Ushahidi dhidi ya Kubenea kuanza kutolewa Jan 20

  mahakama ya kadhi mbona unapaparika sana hata ku-proof read post zako unashindwa ili mradi tu utukane. Kwa hiyo wewe ndiye hakimu

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •