Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  BAADHI YA KUMBUKUMBU MUHIMU ZA UHURU.

  Tanganyika ni jina la kihistoria la sehemu kubwa ya Tanzania ya leo, yaani ile yote isiyo chini ya serikali ya Zanzibar.
  Kwa sababu za kisiasa, mara nyingi huitwa "Tanzania bara" ingawa ina visiwa pia, hasa Mafia na Kilwa.
  Tanganyika ilikuwa eneo lindwa la Uingereza kuanzia 1919 na nchi huru kati ya 1961 hadi 1964, mwaka wa kwanza kama ufalme, halafu kama jamhuri.Mwaka 1964 iliungana na Zanzibar na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Maeneo yaliyoitwa baadaye (1920) "Tanganyika" yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni la Ujerumani lililoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila.
  Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.
  Tangu mwaka 1885 Karl Peters, kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wenyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha na Ukami iliyoweka msingi wa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo hayo.

  Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.
  Koloni lile la Kijerumani lilikuwa kubwa kuliko Tanganyika ya baadaye, maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.

  Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hilo la Kijerumani lilitekwa na majeshi ya Uingereza na Ubelgiji.
  Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua makoloni yote ya Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mikononi mwa Ubelgiji.

  Mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles.
  Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithibitisha hatua hiyo na kuamua masharti ya kukabidhi.
  Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni hilo na tangu Januari 1920 wakaamua kuliita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

  Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961.
  Mwaka 1964 imeunganika na Zanzibar kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Leo hii neno "Tanganyika" latumiwa wakati mwingine kutaja sehemu ya Tanzania isiyo Zanzibar, hasa na watu ambao hawapendi muundo wa serikali mbili tu (ile kuu na ile ya Zanzibar) ndani ya muungano na wanadai kuwa na serikali ya tatu, yaani ile ya Tanganyika.

 2. #2
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: BAADHI YA KUMBUKUMBU MUHIMU ZA UHURU.

  Binadamu wa kwanza kuishi huko huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani, halafu Wabilikimo.Milenia za mwisho Kabla ya Kristo walihamia huko Wakushi kutoka kaskazini, nao wakameza kwa kiasi kikubwa wakazi asili, wakaingiza kilimo, ufugaji na uzalishaji kwa jumla.

  Katika karne za kwanza BK walifika kwa awamu kutoka magharibi wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Nao wakameza kwa kiasi kikubwa wakazi waliotangulia.Hatimaye Waniloti kutoka kaskazini walizidi kuingia hadi karne ya 18.Kabla ya kufika kwa ukoloni kulikuwa na madola madogo mbalimbali na maeneo madogo ya kikabila.Kanda la pwani pamoja na njia za misafara kuelekea Ziwa Tanganyika vilikuwa chini ya athira ya Usultani wa Zanzibar.

  Usultani huo ulikuwa nchi kwenye pwani ya Afrika mashariki kati ya 1856 na 1964.Tangu 1890 ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza.Ilianzishwa wakati wa kugawa Usultani wa Omani mwaka 1856 ikaishia mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzibar na muungano na Tanganyika uliozaa Tanzania.

  Usultani ulianzishwa wakati Sultani Sayyid Said alipoamua kuhamisha makao makuu yake kutoka Maskat (Omani) kwenda Unguja.Sayyid Said alikuwa Sultani wa Omani tangu mwaka 1804. Aliimarisha utawala wa Omani juu ya pwani ya Afrika ya Mashariki.Mwaka 1829 alifaulu kuteka Mombasa iliyokuwa mji pekee wa kujitegemea kati ya miji yote ya Uswahilini.Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa chini ya Omani tangu mwaka 1689, Wareno walipofukuzwa katika pwani za Uswahilini.

  Sayyid Said aliona nafasi kubwa ya biashara ya karafuu kwa ajili ya soko la Uhindi na kwingineko. Mwaka 1829 akaanzisha mashamba ya mikarafuu kwa kutumia kazi ya watumwa kutoka bara.Biashara hiyo ikabadilisha uso wa mji wa Zanzibar wa karne ya 19 uliowahi kuwa kijiji kikubwa tu cha vibanda kando ya boma lililojengwa na Omani kama kizuizi dhidi ya Wareno.Baada ya azimio la mwaka 1832 la kuhamisha mji mkuu wa Omani kwenda Unguja, idadi ya wakazi wa mji ilikua haraka.Nchi za nje zikatambua mji mkuu mpya na kujenga uhusiano. Ubalozi wa Marekani ulijengwa mwaka 1837, Uingereza ukafuata mwaka 1841 na Ufaransa mwaka 1844.Sultani mwenyewe aliondoka kabisa Maskat mwaka 1840. Kukua kwa Zanzibar kulisababisha kukonda kwa mji wa Maskat.

  Baada ya kifo cha Sayyid Sultan mwaka 1856, usultani wa Oman uligawiwa kati ya wanawe. Sayyid Majid bin Said Al-Busaid (1834/1835–1870) akawa Sultani wa kwanza wa Zanzibar na kaka yake Sayyid Thuwaini bin Said al-Said akawa Sultani wa Oman akitawala nchi hiyo bila maeneo ya Afrika ya Mashariki.Usultani mpya ulikuwa nchi yenye nguvu kati ya Rasi Delgado (mpakani na koloni la Kireno ya Msumbiji) hadi Mogadishu (Somalia). Athira yake ilienea kupitia njia za misafara ya pembe za ndovu na watumwa hadi mto Kongo.Wafanyabiashara kama Tippu Tip waliokuwa raia wa Usultani wakapita Tabora na Ujiji kwenda ziwa Tanganyika na kuingia ndani ya eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo. Wapagazi wao walibeba bidhaa kutoka Zanzibar zilizobadilishwa kwa pembe za ndovu hasa. Watumwa walikamatwa au kununuliwa wakabeba pembe hadi pwani.

  Sultani wa pili wa Zanzibar yenyewe, Sayyid Bargash, alijitahidi kujenga uhusiano na nchi za nje. Alifunga soko la watumwa Zanzibar mjini kulingana na mapatano ya kimataifa, lakini akavumilia biashara ya watumwa kuendelea chinichini. Wakati wa Bargash majengo mengi ya Mji Mkongwe yakajengwa.
  Mwishowe mwa utawala wake aliona kupungukiwa kwa eneo lake kutokana na mashindano ya nchi za Ulaya ya kuenea katika Afrika baada ya mkutano wa Berlin.Mwaka 1885 Karl Peters alifanya mikataba ya ulinzi na watawala wadogo waliokuwa chini ya Sultani barani Tanganyika. Upingamizi wa Sultani ulishindikana kwa sababu Wajerumani walituma manowari Unguja akapaswa kukubali maeneo mapya ya Wajerumani.

  Mwaka 1886 mkataba kati ya Uingereza na Ujerumani ulibana eneo la sultani barani katika kanda yenye upana wa maili kumi tu kati ya Rasi Delgado na Mogadishu. Bargash na mfuasi wake Khalifa bin Said waliamua kuuza maeneo hayo au kuyakodisha.1887/1888 pwani ya Kenya ilikodishwa kwa Waingereza. Wakati wa uhuru wa Kenya sehemu hii ikaingizwa katika Jamhuri ya Kenya.Pwani ya Tanganyika ikakodishwa kwa Wajerumani mwaka 1888 na hatimaye kuuzwa mwaka 1890.Miji kwenye pwani ya Somalia ikakodishwa kwa Italia mwaka 1892 ikauzwa mwaka 1906, ila Mogadishu mwaka 1924.Hali halisi usultani ukabaki na visiwa viwili vya Unguja na Pemba tu.Waingereza walikuwa walisita kuhusu Zanzibar lakini baada ya jaribio la Karl Peters la kufanya mkataba na Sultani ili kuingiza visiwa hivyo katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, Uingereza uliamua kutafuta utawala wa visiwa.

  Mkataba wa Zanzibar-Helgoland kati ya Ujerumani na Uingereza ulileta patano la kuwa Zanzibar itakuwa chini ya Uingereza.Tangu mwaka 1890 waziri mkuu wa Sultani alikuwa Mwingereza aliyepokea amri kutoka London.Tangu mwaka 1913 nafasi ilichukuliwa na afisa mkazi mkuu.Kwa muda wa miaka 26 usultani ulikuwa na fedha yake ya pekee iliyoitwa Riali ya Zanzibar.

  Maeneo yaliyoitwa baadaye (1920) "Tanganyika" na baadaye tena Tanzania Bara yaliunganishwa mara ya kwanza tangu mwaka 1886 kama koloni la Ujerumani lililoitwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.Tangu mwaka 1885 Karl Peters, kwa niaba ya Shirika la Ukoloni wa Kijerumani (Gesellschaft für Deutsche Kolonisation) alianza kufanya mikataba na watawala wenyeji katika maeneo ya Usagara, Nguru, Useguha na Ukami iliyoweka msingi wa madai yake ya kuchukua utawala mkuu wa maeneo hayo.Uenezeaji wa Wajerumani uliendelea hasa baada ya kushinda upinzani katika vita ya Abushiri na vita dhidi ya Wahehe.Koloni lile la Kijerumani lilikuwa kubwa kuliko Tanganyika ya baadaye, maana ilijumlisha pia maeneo ya Rwanda na Burundi pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji.Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) koloni hilo la Kijerumani lilitekwa na majeshi ya Uingereza na Ubelgiji.Mkataba wa Versailles wa mwaka 1919 ulikuwa na kanuni za kuchukua makoloni yote ya Ujerumani na kuzikabidhi kwa mataifa washindi wa vita. Sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliwekwa chini ya utawala wa Uingereza, kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi yaliyokabidhiwa mikononi mwa Ubelgiji.

  Mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani, ikiwa na wakazi 3,500,000 hivi, ilikabidhiwa rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles.Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa lilithibitisha hatua hiyo na kuamua masharti ya kukabidhi.Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni hilo na tangu Januari 1920 wakaamua kuliita "Tanganyika Territory" kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki ya eneo.

  Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961.Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Desemba 1963. Uhuru wa usultani ukadumu muda mdogo tu. Mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964 yakamuondoa Sultani. Mauaji ya familia nyingi zenye asili ya Kiarabu yakafuata.Tarehe 26 Aprili 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza (1964-1985) na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais.

  Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.

  Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995-2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa.

  Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005-2015), naye aliendeleza sera yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

  November 5,2015; J P Magufuli aliapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mingine mitano {2015-2020} huku akionekana kuwa na tafauti na mtangulizi wake hasa katika kasi ya utendaji {HAPA KAZI TU.}

 3. #3
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: BAADHI YA KUMBUKUMBU MUHIMU ZA UHURU.

  Hata hivyo unapoizungumzia Tanganyika ni vigumu sana kuitenganisha na Hayati Mwalimu J K Nyerere muaasisi wa Taifa.Huyu ndiye aliweka misingi ya taifa hili, ndiye yeye aliyeandaa jeshi tunaloliona leo, kwa juhudi zake ndiye aliyeanzisha serikali ya mtanganyika ambayo tunayo le na mengine mengi.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tangu 29-10-1964 hadi 05-11-1985.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alizaliwa tarehe 13 Aprili, mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma katika Mkoa wa Mara. Alikuwa mtoto wa Chifu Nyerere Burito na Bibi Christina Mugaya Wanyang’ombe.

  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kuijenga taifa; kudumisha uhuru na amani na kuweka itikadi na sera za kukabili ujinga, umaskini na maradhi. Aidha, awamu hii iliweka misingi madhubuti ya uhusiano wa nje ikiwa ni pamoja na sera ya kutofungamana na siasa za upande wowote, msisitizo katika ukombozi wa Bara la Afrika na mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wao. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Azimio la Arusha lililosisitiza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni matunda ya uongozi wa awamu ya kwanza. Mwalijmu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia katika hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyoko mjini London, Uingereza tarehe 14 Oktoba, 1999. Kutokana na mchango wake mkubwa kama muasisi wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere ataendelea kukumbukwa kuwa Baba wa Taifa.

  Uwezo wa kujieleza na uadilifu vilimsaidia Nyerere kutimiza lengo la TANU la kuipatia nchi uhuru bila vita wala kumwaga damu.Ushirikiano wa Gavana wa Kiingereza Sir Richard Turnbull ulikuwa pia jambo lililochangia kwenye kupata uhuru. Nyerere aliingia
  Baraza la kikoloni la kutunga sheria 1958, na alichaguliwa Waziri Kiongozi 1960. Mwaka 1961, Tanganyika ilipewa uhuru wa madaraka ya ndani na Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza Desemba 9, 1961. Mwaka mmoja badae, Nyerere alichaguliwa Rais wa Tanganyika ilipokuwa Jamhuri. Nyerere aliwezesha muungano kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanganyika kuwa Tanzania, baada ya Mapinduzi ya 1964 yaliyomtoa madarakani Jamshid bin Abdullah, Sultani wa Zanzibar.

  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata elimu ya msingi katika shule ya Mwisenge iliyoko katika Manispaa ya Musoma na baadaye akaendelea na masomo katika shule ya Tabora.

  Alisomea shahada ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda mwaka 1943-45 na mwaka 1952 alihitimu shahada ya uzamili katika masomo ya Historian a Uchumi Edinburgh, Uingereza.

  Baadhi ya nyadhifa alizoshika Mwalimu ni pamoja;

  1954 - Mwanachama Muasisi wa TANU

  1958-1960 - Mbunge wa Bunge la Sheria kwenye uchaguzi wa kwanza ambao waafrika waliruhusiwa kupiga kura

  1958 - Kiongozi wa Upinzani Bungeni

  1960 - Waziri Kiongozi wa Serikali ya ndani

  1961 - Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali Huru ya Tanganyika

  1962 - Alichaguliwa kuwa Rais Tanganyika ilipokuwa Jamhuri

  1963-1970 - Mkuu wa Chuo cha Afrika MAshariki

  1964-1985 - Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

  1970-1985 - Mkuu wa Chuo cha Dar-es-Salaam

  1977-1990 - Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi

  1984-1985 - Mkuu wa Chuo cha Kilimo, Sokoine

  1985 - Alijiuzulu Urais

  1976 - Tuzo ya Nehru kwa maelewano ya kimataifa

  1982 - Tuzo ya Ulimwengu wa tatu

  1983 - Medali ya Nansen huduma iliyotukuka kwa wakimbizi

  1987 - Tuzo ya amani ya Lenin

  1992 - Tuzo ya kimataifa ya Simón Bolívar

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Nov 2015
  Posts
  153
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  13

  Re: BAADHI YA KUMBUKUMBU MUHIMU ZA UHURU.

  Kinachoniumiza mimi kwa habari zinazohusu uhuru, ni kumtaja mtu mmoja tu NYERERE. Mlioandika historia mmetunyima uhuru na nafasi ya kuwafahamu watu wengine walioshiriki kwa ari na mali kutuletea uhuru, matokeo yake ni NYERERE TU, NYERERE TU. Ni kweli alifanya peke yake? Kama hakuwa peke yake hao wengine ni wakina nani? Hivi Sykes hakuwepo kwenye mapambano? WATU MLIOKUWEPO NA MNAOHUSIKA NA KUMBUKUMBU ZA NCHI HAMFANYI VIZURI KATIKA HILI.... Hata Magufuli hafanyi kazi peke yake!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •