Akizungumzia hotuba ya Dk Magufuli, Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema ili afanikiwe kutekeleza sera ya viwanda, dawa pekee ni kuwanyang’anya wawekezaji waliohodhi bila kuviendeleza.Tayari Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru ametoa tangazo la kuwataka wawekezaji walionunua mashamba na viwanda vya Serikali kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mikataba ya mauzo ili kuwabaini waliokiuka masharti.Mikataba yote ya mauzo ya viwanda na mashamba iliyoingiwa kupitia ubinafsishaji, itarejewa upya na kwamba* hatua stahiki zitachukuliwa ikiwamo kurejesha viwanda na mashamba hayo kwenye miliki ya Serikali kwa waliokiuka masharti.