Close

Results 1 to 2 of 2
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2015
  Posts
  221
  Rep Power
  5
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Zitto: ACT - Wazalando itashirikiana na Magufuli

  Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema chama cha ACT-Wazalendo kitashirikiana na Rais John“Nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati za Bunge nimekuwa nikitoa taarifa mbalimbali dhidi wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishaji, sasa tumepata Rais ambaye kaamua kupambana na ufisadi kwa dhati, kaamua kurejesha viwanda vyetu vilivyouzwa ovyo, ni wajibu wetu kumuunga mkono,” ZittoDar/mikoani.*Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema chama cha ACT-Wazalendo kitashirikiana na Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto alisema nchi inanuka uvundo wa ufisadi na kwamba Taifa limepata kiongozi mwenye nia ya dhati ya kupambana nayo kwa dhati na hivyo Watanzania wanalo jukumu la kumuunga mkono.“Nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati za Bunge nimekuwa nikitoa taarifa mbalimbali dhidi wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishaji, sasa tumepata Rais ambaye kaamua kupambana na ufisadi kwa dhati, kaamua kurejesha viwanda vyetu vilivyouzwa ovyo, ni wajibu wetu kumuunga mkono,” alisema. *Alisema asilimia 60 ya masuala yaliyotajwa na Rais Magufuli katika hotuba yake yanatoka kwenye ilani ya ACT ambayo walimkabidhi wakati alipotangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.Akizungumzia kitendo cha Zitto kutoungana na wabunge wa Ukawa kususia hotuba ya Rais, mshauri wa ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo alisema huo ni msimamo wa chama hicho kwa kuwa matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa kwa njia za kisheria na kisiasa.Alisema chama hicho kinamtambua Dk Magufuli kama mshindi halali wa kiti cha urais.“Katika hili la Zanzibar tunafanana katika msingi wa hoja lakini tunatofautiana katika mkakati wa utekelezaji wa hoja husika na hili halina ubaya wowote, ni afya kabisa kwa demokrasia yetu,” alisema Mkumbo.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2015
  Posts
  444
  Rep Power
  5
  Likes Received
  6
  Likes Given
  3

  Re: Zitto: ACT - Wazalando itashirikiana na Magufuli

  huyu yuda tu

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •