Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  473
  Rep Power
  6
  Likes Received
  10
  Likes Given
  6

  NANI KAMA WAZIRI MKUU MAJALIWA ?

  WANANCHI na wasomi wa Ruangwa na Dodoma, wanaamini Tanzania imepata kiongozi anayefahamu changamoto zinazowakabili watanzania wa hali ya kawaida kutokana na uteuzi wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Wasomi na wananchi hao walimpongeza Rais John Magufuli kwa kumteua Mbunge wa Ruangwa, mkoani Lindi, Kassim Majaliwa na kuongeza kuwa rais hajapotea kwani amechagua mtu sahihi anayeweza kusimamia na kusaidia wananchi.Wanasema hivyo kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake yaani mwaka 2010 hadi 2015 amefanya kazi mbalimbali za maendeleo katika jimbo hilo pamoja na kuisaidia wilaya hiyo changa iliyoanzishwa baada ya kugawanywa wilaya ya Lindi na kuzinduliwa rasmi na Rais mstaafu Benjamin William Mkapa.Wananchi hao waliainisha kwa uchache mambo ambayo Majaliwa alifanya kwa wapigakura wake wakati akiwa mbunge na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi-Elimu).Kwa mujibu wa wananchi hao baadhi ya mambo aliyofanya ni pamoja na kutenga Sh milioni tano kila mwaka kwa ajili ya vijana waliofaulu darasa la saba kwenda sekondari, lakini wakashindwa kwenda kuanza shule ambapo hadi sasa vijana 372 wamejiunga sekondari, alipunguza tatizo la vitabu mashuleni kwa kusambaza vitabu katika shule za msingi 38 na shule zote za sekondari 15 vya masomo ya sanaa na sayansi.Mambo mengine aliyofanya mbunge huyo ilikuwa kufadhili kuanzishwa kwa maktaba yenye hadhi ya wilaya yenye vitabu 7,000 na uwezo wa mtu yeyote kujiendeleza kwa nyanja tofauti ambayo ilizinduliwa Novemba 2011, alisambaza vifaa vya maabara ya masomo ya sayansi (fizikia, kemia na bayolojia) katika shule zote za sekondari 15 pamoja na kuanza kwa shule ya kidato cha tano na sita ya Mbekenyera na sasa anakamilisha kuiandaa Shule ya Sekondari Nkowe iwe ya pili na tayari kuna milioni 200 ambazo zinatumika kujenga mabweni mawili.Majaliwa amewezesha kupatikana kwa maabara za kompyuta 20 katika shule za Mbekenyera, Nkowe, na sasa Mnacho Sekondari na kwamba msaada huo umenufaisha shule za ndani ya Mkoa huo kama Ilulu, Lindi, Mahiwa, Kilwa na Ng’apa, amewezesha kujengwa shule ya msingi Chikundu ambayo iliezuliwa na kimbunga.Katika sekta ya afya pia, Majaliwa amefanya mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa magodoro 100 na shuka 200 katika Hospitali ya Wilaya, Kituo cha Afya Mandawa na Kituo cha Afya Nkowe, aliwezesha kupata madaktari 35 bingwa wa kutibu macho bure kutoka India na wananchi 3,800 walinufaika, aliwezesha kupata madaktari watano bingwa wa kutibu matende bure wamemaliza kazi, sambamba na kuwezesha kupata ufadhili wa gari ya wagonjwa mpya kutoka nchini Korea.Kutoka Dodoma, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma Tanzania (ASAs), Paul Loisulie amesema uteuzi wa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu umekuwa ni bora zaidi kwani ni mtu mnyenyekevu ambaye anaweza kuisaidia nchi kusonga mbele. Loisulie, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema hayo jana wakati wa mahojiano na kubainisha kuwa Majaliwa siyo mtu wa kujivuna asiye na makundi.Alisema anakubaliana na uteuzi huo na Rais Magufuli.“Binafsi nakubaliana na uteuzi kwa sababu tatu, sababu ya kwanza kuna watu wangepewa ningesikitika sana, ukimlinganisha na wengine waliokuwa wanatajwa huyu ana nafuu,” alisema.Alisema alibahatika kumfahamu Waziri Mkuu Majaliwa wakati akifanya utafiti bungeni, na walikuwa wakihoji wabunge tofauti na wabunge wengine hata wa upinzani. “Majaliwa ni mnyenyekevu mno akikupa ahadi anatekeleza.Tulimpigia simu alikuwa nje ya Dodoma hakupokea lakini baadae akapiga mwenyewe na alipokuja Dodoma alitutafuta yeye tukamhoji, baadhi ya wabunge wengine walikuwepo Dodoma lakini hata kuongea nae ni shida, mtu mnyenyekevu anaweza kuisaidia nchi hii,” alisema.Kwa upande wake ofisa tarafa wa Itiso Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Remidius Emmanuel alisema binafsi hakutegemea kama Majaliwa atateuliwa kuwa waziri mkuu.“Sikutegemea lakini kimsingi inadhihirisha hali aliyoanza nayo Rais Magufuli ile dhana ya hapa kazi tu na ule utofauti wake kiutendaji sasa unaonekana kwani anachoangalia ni utendaji wa mtu na umakini wake”.Alisema hata Waziri Mkuu alikuwa hafahamu kuwa jina lake ndilo lilikuwa kwenye bahasha kabla ya kusomwa bungeni.Alisema kutokana na uteuzi huo anaamini hata baraza la mawaziri litakuwa ni tofauti na litapatikana baraza ambalo hakuna aliyelifikiria.Mkazi wa Kisasa Subira Waziri alisema anaamini serikali ya awamu chini ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa itasaidia kuwaletea wananchi maendeleo na kupunguza pengo lililopo kama ya wenye nacho na wasio nacho.Alisema sasa kumekuwa na pengo kubwa kwa masikini na matajiri na hilo litawezekana kama kutakuwa na mipango kabambe ya kuanzishwa kwa viwanda ambavyo vitasaidia kuongeza ajira.Alisema kwenye maeneo ambayo yana uzalishaji mkubwa wa mazao kama ufuta alizeti na karanga viwanda vijengwe katika maeneo hayo ili wananchi wapate ajira na kuinua hali zao za maisha na si kufikiriwa kujengwa kwa viwanda maeneo ya mijini tu

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2015
  Posts
  436
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: NANI KAMA WAZIRI MKUU MAJALIWA ?

  hakika atawasaidia sana wananchi kama kweli ataendeleza hiyo juhudi aliyoifanya huko lindi

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: NANI KAMA WAZIRI MKUU MAJALIWA ?

  Nampa muda maana hawa hawaaminiki

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2015
  Posts
  444
  Rep Power
  5
  Likes Received
  6
  Likes Given
  3

  Re: NANI KAMA WAZIRI MKUU MAJALIWA ?

  ngoja tuone maana ndio walivyo hao

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •