Abiria wakwama barabarani kwa saa 48 Kenya

Maafisa wa polisi wa trafiki wametumwa ili kujaribu kumaliza msongamano wa magari ambao umechukua siku mbili katika barabara kuu ya Mombasa Nairobi.
Barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa jimbo hilo kwa kuwa inaunganisha bandari ya Mombasa na mataifa yasiokuwa na Bandari.
Eneo lililoathiriwa pakubwa ni lile la Taru,yapata kilomita 80 kutoka Mombasa.

Waandishi wanasema kuwa msongamano huo umesababishwa na marekebisho yanayofanywa katika barabara kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Milolongo mirefu ya magari huwa jambo la kawaida nchini Kenya na haswa husababishwa na barabara mbovu ambazo hazirekebishwi.
Mabasi ya abiria na malori yanayobeba mizigo na kupeleka Nairobi na kwengineko ni miongoni mwa magari yaliokwama tangu mlolongo huo uanze siku ya jumanne jioni.