Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  466
  Rep Power
  7
  Likes Received
  25
  Likes Given
  1

  TETESI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.

  Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung ano wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  4 Novemba, 2015

 2. #2
  Senior Member Mshangai's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  188
  Rep Power
  7
  Likes Received
  18
  Likes Given
  13

  Re: TETESI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Hajafanya uteuzi tena?

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: TETESI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Tumeambiwa kesho sikuku ila hatujajua ambiwa sikuku gani

 4. #4
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: TETESI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Sikukuu ya uchakachuzi

 5. #5
  Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  33
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: TETESI: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Kesho tutakuwa tukishuhudia ushindi wa dhuluma dhidi ya haki.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •