Close

Results 1 to 19 of 19
 1. #1
  Senior Member Tumbo's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Location
  Tanzania
  Posts
  358
  Rep Power
  6
  Likes Received
  18
  Likes Given
  22

  MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KURA.

  Wasalaam wadau,
  Kama mnavyo jua zimebaki siku 5 kabla uchaguzi mkuu hapo October 25th, hivi karibuni hiyo NEC imebandika majina ya wapiga kura kwenye vituo walivyo jiandikisha ili wananchi wakahakiki na kukagua majina yao.

  Kabla ya kubandika majina hayo vyama vya upinzani hususan Chadema / Ukawa wamekuwa wakishinikiza NEC kutoa nakala tete ya majina ya wapiga kura walioandikishwa na NEC, hata NEC waliitoa hiyo copy kwa wadau lakini ikaja bainika ina makosa mengi sana, na baadae kuyabandika vituoni kwa ajili ya wananchi kuhakiki ili wasikose fursa na haki ya kupiga kura.

  Ni bahati mbaya sana wengi wamekuwa wakilalamika kwa kutokuona majina yao katika vituo hivo walivyo jiandikishia hali itakayo wanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowapenda, kwa kuthibitisha hilo leo jioni nami nikapata mda nikasema ngoja niende kituo nilipojiandikisha nikahakiki jina langu, kwa bahati mbaya sana jina langu sikuliona na nikakuta watu wengi tu hapo kituoni ambao pia hawakuona majina yao, na hakuna wa kumuuliza. Kuna namba NEC wametoa kwa msaada ambayo ni *152*00# sms na 0800782100 kwa voice calls, baada ya kutoona jina langu nimetuma sms kufuata maelekezo nikapokea ujumbe kuwa swala langu linashughulikiwa hivyo ntapokea ujumbe baada ya mda mfupi.

  Kama hiyo haitoshi nimepiga simu ili kupata msaada au maelekezo ya nini cha kufanya aidha hatua ya kufuata lakini mda wote hiyo simu haikuwa hewani, Je hizo si hujuma dhidi ya democracy? Je haya si mazingira ya BAO la MKONO? Hatima yangu na wengine ni nini na siku zenyewe ndo zinayoyoma? Ndo nishakosa haki yangu ya msingi na ya kikatiba?
  HAKI ikitendeka, AMANI hutamalaki, hakuna AMANI pasipo HAKI.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Pole sana,NEC haijafanya hayo kwa bahati mbaya.Ni maandalizi ya goli la mkono ambayo UKAWA imekuwa ikiyapigia kelele kila siku.Katika hali ya kawaida haiwezekani majina yatolewa siku nane kabla ya uchaguzi halafu utegemee maboresho yatafanyika kwa kipindi hicho kifupi kilichosalia.HAIWEZEKANI.

  Kuna watu wanaishi katika maeneo ambayo hayana hata mawasiliano.Watu kama hao watafanyaje kama majina yao hayaonekani.NI MAANDALIZI YA GOLI LA MKONO.

  Pia NEC wanachotaka kukifanya hapa ni kuruhusu watu wote wenye kadi za kupigia kura wapige kura bila kujala kama majina yao yapo kwenye daftari la wapiga kura kwa kisingizio kuwa muda wa maboresho hautatosha.HAPO NDIPO UWEZEKANO WA KUINGIZA KADI FEKI( kura hewa) unapoweza kutokea.UKAWA wasiruhusu hilo.

  Vile vile UKAWA wawe makini na aina hii ya goli la mkono.Kwamba,mimi naamini watakaopiga kura hawatazidi asilimia 70 ya waliojiandikisha.Hawa jamaa wanaweza kutumia udhaifu huo kuongeza kura hewa asilimia fulani au kulingana na mahitaji ya ushindi wa hao wanaowabeba na baadae kuja na takwimu za uongo za waliopiga kura.

  Ni muhumu kwa UKAWA kuhakikisha wanapata matokeo yote mapema toka kwenye vituo ,na mawakara wao kuwa makini wakati wote HASA KIPINDI CHA KUHESABU KURA.
  Last edited by Nyaluhala; 21-10-2015 at 09:50.

 3. #3
  Moderator
  Join Date
  Apr 2015
  Posts
  1,067
  Rep Power
  6
  Likes Received
  21
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Viongozi watanzania hawana uzalendo na nchi yao ila ni wazalendo wa matumbo yao huwa napatas wakati mgumu wanavyo ipeleka nchi hii utazani wanafanya kazi ya mzungu sasa unapo pitisha kiongozi mbaya athari ni kwa tanzania kiongozi mzuri maendeleo ni ya Tanzania sasa viongozi viongozi wabovuv wa nini?

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  497
  Rep Power
  5
  Likes Received
  8
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Hili suala la wananchi kuotkuona majina yao katik vituo vya kupigia kura limejitokeza sehemu nyingi sana hasa kwa jiji hili la dar es salaam ambapo nami ni miongoni wa wahanga wa tatizo hili na ni isharatosha kabisa ya kutengeneza bao lamkono, hivi kwanini wanatunyima haki zetu za msingi za kumtafuta kiongozi anayetufaa kwa mwendo huu nchi yetu haitokuja pata maendeleo hata cku moja labda ashuke malaika aje atusaidie na viongozi wamekaa kimya kabisa hata hawathubutu kuongelea tatizo hili au kutupa njia za kutatua na ukicheki zimebaki cku chache za kwenda kupiga kura

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2015
  Posts
  441
  Rep Power
  5
  Likes Received
  4
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Ujinga ulio fanywa katika jimbo la ubungo niwakuukemea sio wakuvumilika inakuwaje majina yawatu walio jiandikisha ni machache na yaliyo letwa na tume ni mengi sasa hii tume tuiitaje bado sana kuwa na tume huru

 6. #6
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2015
  Posts
  221
  Rep Power
  5
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Nec naona kama inatengeneza hilo bao la mkono maana hata siwaelewii

 7. #7
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2015
  Posts
  436
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  wao watengeneze wasitengenezeilo bao lao cjui la kidole au mkono ila wajue Lowasa ni raisi

 8. #8
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2015
  Posts
  444
  Rep Power
  5
  Likes Received
  6
  Likes Given
  3

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  NEC bila kuwa macho huo CCM watazurumu haki ya watanzania

 9. #9
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Aliye iteua NEC ni raisi ndio huyo huyo anaye wafukuza raia waende majumbani mwao ilikitoktee nn?

 10. #10
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  238
  Rep Power
  5
  Likes Received
  2
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  NEC mnatuangusha jamani

 11. #11
  Moderator
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  599
  Rep Power
  5
  Likes Received
  7
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  NEC naomba uchaguzi uwe wa haki na amani maana mnaweza kuleta machafuko kwa kuonyesha upendeleo wa upande wowote

 12. #12
  Senior Member Tumbo's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Location
  Tanzania
  Posts
  358
  Rep Power
  6
  Likes Received
  18
  Likes Given
  22

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Kwa kweli nimeumia sana, kwani nimefanya kazi kubwa mtaani kwangu na kila nilipo pita kuhamasisha watu katika harakati za M4C, nimewashawishi wengi tu kuchagua mabadiliko mwisho wa siku mimi sipigi kura...! Kwa kweli hii siyo fair.

  Leo asubuhi nimefutilia hili swala katika ofisi za kata huko napo mizinguo hata hakuna anayenijali mwisho wa siku naambiwa niangalie kwenye cm, kwa namba *150*00# nilipo angalia cha ajabu NAMBA ya KITAMBULISHO changu imekuja na jina lingine ambalo sio langu, na kituo chake cha kupiga kura ni mbweni.

  Kipindi cha kuhakiki majina kipindi kilee nilienda kuhakiki jina langu katika ofisi za kata na jina langu nikaliona na halikua na tatizo lolote nashangaa leo hii imekuaje nini kimebadilika..?! Nimechukia sana, nitoe rai kwa wote mtakao pata fursa ya kupiga kura msifanye makosa, tunahitaji mabadiliko pigeni kura kwa wingi muiondoe hili jinamizi na makaburu miccm, mimi nitashiriki kulinda kura.
  HAKI ikitendeka, AMANI hutamalaki, hakuna AMANI pasipo HAKI.

 13. #13
  Senior Member Tumbo's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Location
  Tanzania
  Posts
  358
  Rep Power
  6
  Likes Received
  18
  Likes Given
  22

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Meimei,
  Wewe ni gamba la wapi kila mara unaandika lugha isiyoeleweka kwa wengi? Mara nyingi umekua ukiniandikia private message kwa lugha ambayo siielewi una maana gani ndugu? Lugha zinazo ruhusiwa ni Kiswahili na kiingereza kama huzielewi ni bora ukabaki kuwa msomaji na si mchangiaji.
  HAKI ikitendeka, AMANI hutamalaki, hakuna AMANI pasipo HAKI.

 14. #14
  Senior Member Erasmus's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  406
  Rep Power
  6
  Likes Received
  7
  Likes Given
  3

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Kamanda Tumbo, pole sana kwa hayo yaliyokukuta. NEC/Serikali ndio wanatakiwa kubeba lawama. Kwa nini daftari halikutolewa mapema ili kuwa na muda wa kutosha wa kushughulikia na kurekebisha dosari hizi?
  UKWELI UTAKUWEKA HURU DAIMA

 15. #15
  Senior Member Erasmus's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  406
  Rep Power
  6
  Likes Received
  7
  Likes Given
  3

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Moderator, huyo 'meimei' mbona mnamuacha anatangaza biashara ya viagra humu?
  UKWELI UTAKUWEKA HURU DAIMA

 16. #16
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2015
  Posts
  436
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  hehehehehehehehehehehe kumbe

 17. #17
  Moderator
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  599
  Rep Power
  5
  Likes Received
  7
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  JAJI LUBUVA NA TUME YAKO YA NEC!!!!! tendeni haki kwa manufaa ya watanzania

  - - - Updated - - -

  JAJI LUBUVA NA TUME YAKO YA NEC!!!!! tendeni haki kwa manufaa ya watanzania

 18. #18
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2015
  Posts
  436
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Haki isipotendeka watasababisha amani ya tanzania kutoweka, watanzania wataihitaji gharama kuitafuta haki yao, kwa hiyo NEC tunawaomba haki itendeke kwa usawa

 19. #19
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: MAZINGIRA YA BAO LA MKONO, NEC NA HUJUMA DHIDI YA DEMOCRACY NA HAKI YA KUPIGA KUR

  Quote Originally Posted by Tumbo View Post
  Wasalaam wadau,
  Kama mnavyo jua zimebaki siku 5 kabla uchaguzi mkuu hapo October 25th, hivi karibuni hiyo NEC imebandika majina ya wapiga kura kwenye vituo walivyo jiandikisha ili wananchi wakahakiki na kukagua majina yao.

  Kabla ya kubandika majina hayo vyama vya upinzani hususan Chadema / Ukawa wamekuwa wakishinikiza NEC kutoa nakala tete ya majina ya wapiga kura walioandikishwa na NEC, hata NEC waliitoa hiyo copy kwa wadau lakini ikaja bainika ina makosa mengi sana, na baadae kuyabandika vituoni kwa ajili ya wananchi kuhakiki ili wasikose fursa na haki ya kupiga kura.

  Ni bahati mbaya sana wengi wamekuwa wakilalamika kwa kutokuona majina yao katika vituo hivo walivyo jiandikishia hali itakayo wanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowapenda, kwa kuthibitisha hilo leo jioni nami nikapata mda nikasema ngoja niende kituo nilipojiandikisha nikahakiki jina langu, kwa bahati mbaya sana jina langu sikuliona na nikakuta watu wengi tu hapo kituoni ambao pia hawakuona majina yao, na hakuna wa kumuuliza. Kuna namba NEC wametoa kwa msaada ambayo ni *152*00# sms na 0800782100 kwa voice calls, baada ya kutoona jina langu nimetuma sms kufuata maelekezo nikapokea ujumbe kuwa swala langu linashughulikiwa hivyo ntapokea ujumbe baada ya mda mfupi.

  Kama hiyo haitoshi nimepiga simu ili kupata msaada au maelekezo ya nini cha kufanya aidha hatua ya kufuata lakini mda wote hiyo simu haikuwa hewani, Je hizo si hujuma dhidi ya democracy? Je haya si mazingira ya BAO la MKONO? Hatima yangu na wengine ni nini na siku zenyewe ndo zinayoyoma? Ndo nishakosa haki yangu ya msingi na ya kikatiba?
  Ndio maana rasimu ya katiba ya warioba ilitaka tume iwe ya haki kwa kuepuka mambo kama haya

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •