Close

Results 1 to 14 of 14
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,227
  Rep Power
  9
  Likes Received
  73
  Likes Given
  3

  Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limetoa ripoti ya kile kilichoelezwa kuwa ni sababu zilizopelekea ajali iliyopelekea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mch. Christopher Mtikila na kuainisha sababu hizo kuwa ni pamoja na:
  1. Ubovu wa gari kwa kuwa lilipata ajali oktoba 3, moja ya sehemu muhimu zilizoharibika ni mfumo wa usukani, hivyo inawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia ajali hiyo ya pili.
  2. Mtikila kutovaa mkanda wa usalama na hivyo kusababishwa arushwe nje kupitia kioo cha mbele.
  3. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu ya kuendesha gari mchana na usiku na kabla ya safari kurudi alikuwa akishughulikia matengenezo ya gari hivyo hakupata muda wa kumpumzika.
  4. Mwendo kasi.

  maswali tata baada ya ripoti ya Polisi
  1. Kutofunga Mkanda na hivyo kurushwa nje kupitia kioo cha mbele ni sababu ya ajali au ni yatokanayo na ajali hiyo?
  2. Mwili wa Mch. Mtikila haukua na jeraha sehemu yoyote ya mwili, unaweza kurushwa nje kupitia kioo cha mbele hata usichubuke? Ripoti ya Daktari inasema marehemu alivunjika mbavu nane, unaweza kuvunjika mbavu 8 bila kujibamiza popote? Na kama alijibamiza, unaweza kujibamiza na jeraha lisionekane?
  3. Mtikila amesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Njombe na kurudi kuja kupata ajali Mkoani Pwani. Mbona ripori ya ya kifo chake imetolewa Mapema sana isivyozoeleka?
  4. Daktari aliyechunguza safari za kifo chake ni wa Hospitali ya Tumbi alikopelekwa mara ya kwanza au wa *Muhimbili alikohamishiwa?

  Kifo cha Mtikila kimekuja baada ya Serikali ya Rwanda inayoongozwa na rais Paul Kagame, rais anayetajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa kushutumu Mtikila kumpa hifadhi kiongozi wa jeshi la waasi la FDLR nchini humo, Brigedia Jenerali GRATIEN KABILIGI( http://www.newsofrwanda.com/featured...ictr-convicts/ )
  Aidha, tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM ambapo Lowassa naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro na hata alipohamia Ukawa, Mtikila amempinga waziwazi kuwa hana sifa za kwenda ikulu kwa sababu ya ufisadi na afya yake. Mtikila alitoa waraka unaosomeka"MTIKILA ATOA WARAKA MKALI KUMHUSU LOWASSA, ADAI NI BALAA"(http://www.chahali.com/2015/07/urais...aka-mkali.html )

  Mambo hayo mwili yanahusishwa na kifo cha Mch. Mtikila hususan kupitia mitandao ya kijamii. Watu wamekwenda mbali na kusema namna ambavyo mwili wa Marehemu Mtikila ulivyokuwa umelazwa ndivyo hulazwa maiti za watu waliyouwawa kwa sababu ya kuikosoa serikali ya Kagame.

 2. #2
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Haya maswali yako tata kwa nini usimuulize Ernest Mangu? Mbona mnahangaika sana au ninyi ndiyo mumemuua sasa damu yake inaanza kuwatesa? Kwa sababu ni kawaida yenu kuchochea migogoro ikishafika kileleni mnamtoa roho mtu ili upande mwingine upate lawama. Nakumbuka mlifanya hivyo kwa Chacha Wangwe mgogoro ulpokomaa makamtoa roho kwa staili hii halafu haraka mkatengeneza riport ya uongo mkampa Mtikila aisambaze kwenye vyombo vya habari kuwa Mbowe na Reginld mengi ndiyo walikodi wauaji toka Kenye kuja kumuua Chacha. Hata hili lazima ccm na vitengo vyenu mnahusika kwani staili mliyotumia ni ile ile.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Feb 2015
  Posts
  473
  Rep Power
  6
  Likes Received
  10
  Likes Given
  6

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  mzee nenda polisi kaulizie hio ripoti vizuri mwili wa marehemu unamajelaa kichwani na miguuni japo sio majeraha makubwa na pia aliumia ndani kwa ndani sasa sijui wewe hio ripoti yako umeitowa wapiii

 4. #4
  Moderator
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  599
  Rep Power
  5
  Likes Received
  7
  Likes Given
  0

  Quote Originally Posted by TataMadiba View Post
  Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limetoa ripoti ya kile kilichoelezwa kuwa ni sababu zilizopelekea ajali iliyopelekea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mch. Christopher Mtikila na kuainisha sababu hizo kuwa ni pamoja na:
  1. Ubovu wa gari kwa kuwa lilipata ajali oktoba 3, moja ya sehemu muhimu zilizoharibika ni mfumo wa usukani, hivyo inawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia ajali hiyo ya pili.
  2. Mtikila kutovaa mkanda wa usalama na hivyo kusababishwa arushwe nje kupitia kioo cha mbele.
  3. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu ya kuendesha gari mchana na usiku na kabla ya safari kurudi alikuwa akishughulikia matengenezo ya gari hivyo hakupata muda wa kumpumzika.
  4. Mwendo kasi.

  maswali tata baada ya ripoti ya Polisi
  1. Kutofunga Mkanda na hivyo kurushwa nje kupitia kioo cha mbele ni sababu ya ajali au ni yatokanayo na ajali hiyo?
  2. Mwili wa Mch. Mtikila haukua na jeraha sehemu yoyote ya mwili, unaweza kurushwa nje kupitia kioo cha mbele hata usichubuke? Ripoti ya Daktari inasema marehemu alivunjika mbavu nane, unaweza kuvunjika mbavu 8 bila kujibamiza popote? Na kama alijibamiza, unaweza kujibamiza na jeraha lisionekane?
  3. Mtikila amesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Njombe na kurudi kuja kupata ajali Mkoani Pwani. Mbona ripori ya ya kifo chake imetolewa Mapema sana isivyozoeleka?
  4. Daktari aliyechunguza safari za kifo chake ni wa Hospitali ya Tumbi alikopelekwa mara ya kwanza au wa *Muhimbili alikohamishiwa?

  Kifo cha Mtikila kimekuja baada ya Serikali ya Rwanda inayoongozwa na rais Paul Kagame, rais anayetajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa kushutumu Mtikila kumpa hifadhi kiongozi wa jeshi la waasi la FDLR nchini humo, Brigedia Jenerali GRATIEN KABILIGI( EXCLUSIVE: Tanzania hosts more meetings for FDLR with ICTR convicts News Of Rwanda ? Rwanda News )
  Aidha, tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM ambapo Lowassa naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro na hata alipohamia Ukawa, Mtikila amempinga waziwazi kuwa hana sifa za kwenda ikulu kwa sababu ya ufisadi na afya yake. Mtikila alitoa waraka unaosomeka"MTIKILA ATOA WARAKA MKALI KUMHUSU LOWASSA, ADAI NI BALAA"(#Urais 2015: Mtikila atoa waraka mkali sana kuhusu Lowassa, adai ni balaa kwa taifa ~ Kulikoni Ughaibuni )

  Mambo hayo mwili yanahusishwa na kifo cha Mch. Mtikila hususan kupitia mitandao ya kijamii. Watu wamekwenda mbali na kusema namna ambavyo mwili wa Marehemu Mtikila ulivyokuwa umelazwa ndivyo hulazwa maiti za watu waliyouwawa kwa sababu ya kuikosoa serikali ya Kagame.
  Nahisi mnaikosoa mipango ya mungu mtikila nae ni binadam, Mtu amekufa kwa ajari na imeonekana je angekufa akiwa amelala kwake sindio mngeandamana

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  9
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Polisi wamejichanganya sana. Labda mkono wa mafisadi uliwatembelea

  - - - Updated - - -

  Kelvin, kwani na kifo cha Chacha Wangwe unasema kuwa ilikuwa ni mipango ya Mungu? Kama ndo hivyo, kwa nini huyo Mungu katika amri zake 10 hususan amri ya 5 alisema USIUE?

 6. #6
  Senior Member mahakama ya kadhi's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  993
  Rep Power
  7
  Likes Received
  31
  Likes Given
  31

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Mafisadi wamemuuwa mtikila wetu lakini mahakama ya mafisadi inakuja tutawanyoosha tu.

 7. #7
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  9
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Quote Originally Posted by Aggrey Lugano View Post
  mzee nenda polisi kaulizie hio ripoti vizuri mwili wa marehemu unamajelaa kichwani na miguuni japo sio majeraha makubwa na pia aliumia ndani kwa ndani sasa sijui wewe hio ripoti yako umeitowa wapiii
  Hata Chacha Wangwe mlisema vivyo hivyo ila ikaja kuthibitika baadaye kuwa aliuawa.

 8. #8
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2015
  Posts
  436
  Rep Power
  5
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Quote Originally Posted by TataMadiba View Post
  Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limetoa ripoti ya kile kilichoelezwa kuwa ni sababu zilizopelekea ajali iliyopelekea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mch. Christopher Mtikila na kuainisha sababu hizo kuwa ni pamoja na:
  1. Ubovu wa gari kwa kuwa lilipata ajali oktoba 3, moja ya sehemu muhimu zilizoharibika ni mfumo wa usukani, hivyo inawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia ajali hiyo ya pili.
  2. Mtikila kutovaa mkanda wa usalama na hivyo kusababishwa arushwe nje kupitia kioo cha mbele.
  3. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu ya kuendesha gari mchana na usiku na kabla ya safari kurudi alikuwa akishughulikia matengenezo ya gari hivyo hakupata muda wa kumpumzika.
  4. Mwendo kasi.

  maswali tata baada ya ripoti ya Polisi
  1. Kutofunga Mkanda na hivyo kurushwa nje kupitia kioo cha mbele ni sababu ya ajali au ni yatokanayo na ajali hiyo?
  2. Mwili wa Mch. Mtikila haukua na jeraha sehemu yoyote ya mwili, unaweza kurushwa nje kupitia kioo cha mbele hata usichubuke? Ripoti ya Daktari inasema marehemu alivunjika mbavu nane, unaweza kuvunjika mbavu 8 bila kujibamiza popote? Na kama alijibamiza, unaweza kujibamiza na jeraha lisionekane?
  3. Mtikila amesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Njombe na kurudi kuja kupata ajali Mkoani Pwani. Mbona ripori ya ya kifo chake imetolewa Mapema sana isivyozoeleka?
  4. Daktari aliyechunguza safari za kifo chake ni wa Hospitali ya Tumbi alikopelekwa mara ya kwanza au wa *Muhimbili alikohamishiwa?

  Kifo cha Mtikila kimekuja baada ya Serikali ya Rwanda inayoongozwa na rais Paul Kagame, rais anayetajwa kuwa na mawasiliano ya karibu na mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa kushutumu Mtikila kumpa hifadhi kiongozi wa jeshi la waasi la FDLR nchini humo, Brigedia Jenerali GRATIEN KABILIGI( EXCLUSIVE: Tanzania hosts more meetings for FDLR with ICTR convicts News Of Rwanda ? Rwanda News )
  Aidha, tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM ambapo Lowassa naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro na hata alipohamia Ukawa, Mtikila amempinga waziwazi kuwa hana sifa za kwenda ikulu kwa sababu ya ufisadi na afya yake. Mtikila alitoa waraka unaosomeka"MTIKILA ATOA WARAKA MKALI KUMHUSU LOWASSA, ADAI NI BALAA"(#Urais 2015: Mtikila atoa waraka mkali sana kuhusu Lowassa, adai ni balaa kwa taifa ~ Kulikoni Ughaibuni )

  Mambo hayo mwili yanahusishwa na kifo cha Mch. Mtikila hususan kupitia mitandao ya kijamii. Watu wamekwenda mbali na kusema namna ambavyo mwili wa Marehemu Mtikila ulivyokuwa umelazwa ndivyo hulazwa maiti za watu waliyouwawa kwa sababu ya kuikosoa serikali ya Kagame.
  JAMANI MTIKILA SIO MALAIKA NA YEYE NI BINADAMU, HEBU ACHENI KUWAZA VITU AMBAVYO HAVIPO KILA MMOJA LAZIMA AONJE UMAUTI

 9. #9
  Member Tisi's Avatar
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  53
  Rep Power
  7
  Likes Received
  1
  Likes Given
  5

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Quote Originally Posted by Kelvin Mwaipungu View Post
  Nahisi mnaikosoa mipango ya mungu mtikila nae ni binadam, Mtu amekufa kwa ajari na imeonekana je angekufa akiwa amelala kwake sindio mngeandamana
  bosi watu hawakatai kifo ila lazima watueleze vizuri isiwe sababu ya kifo kuwa lazima kila mtu afe ndio tusihoji amekufaje huu ni ukosefu wa kufikiri lazima tuhoji ili hii nchi tusiiifanye na machinjuio ya binaadamu wenzetu
  afrika bila ya ushoga inawezekana

 10. #10
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  2,802
  Rep Power
  7
  Likes Received
  89
  Likes Given
  66

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Pelekeni ushaidi wa kifo chake mahakamani msiongee kwenye mitandao

 11. #11
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  hata baada ya uchaguzi naomba hiyo ishu ya Mtikila iende mahakamani ikiwa sivyo mta kuwa mnataka kuchafua Lowassa hilo lengo lenu lime buma

 12. #12
  Senior Member
  Join Date
  Mar 2015
  Posts
  441
  Rep Power
  6
  Likes Received
  4
  Likes Given
  0

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Quote Originally Posted by Nambalapala View Post
  Hata Chacha Wangwe mlisema vivyo hivyo ila ikaja kuthibitika baadaye kuwa aliuawa.
  Mambo mnayo yafanya yata wagharimu huko tuendako matukio mfanye ninyi msingizie wengine

 13. #13
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2015
  Posts
  238
  Rep Power
  5
  Likes Received
  2
  Likes Given
  0

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  acheni kuhisihisi vitu, mmekuwa watu wa kuhisi huyu kafanya hiki yule kafanya kile, hebu tutoke kwenye mawazo mgando

 14. #14
  Moderator
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  599
  Rep Power
  5
  Likes Received
  7
  Likes Given
  0

  Re: Maswali tata baada ya ripoti ya Polisi kuhusu kifo cha Mch. Mtikila

  Quote Originally Posted by Nambalapala View Post
  Polisi wamejichanganya sana. Labda mkono wa mafisadi uliwatembelea

  - - - Updated - - -

  Kelvin, kwani na kifo cha Chacha Wangwe unasema kuwa ilikuwa ni mipango ya Mungu? Kama ndo hivyo, kwa nini huyo Mungu katika amri zake 10 hususan amri ya 5 alisema USIUE?

  Ndio upeleke ushaidi wa kifo cha mtikila mahakamani

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •