Mazingira ya kifo cha Mchungaji Mtikila bado
kinatia shaka kuu mbele ya jamii na nachelea
kusema huyu Mzee ameuawa na genge la mafisadi
ili wafanikiwe kisiasa kwani Mtikila alikuwa
ameshakusanya vielelezo vyote vya
kuwashughulikia.
1. Jeshi la Polisi Watanzania tunaomba mtusaidie
kumuhoji kwa kina huyu mtu anaeitwa Mchungaji
Patrick Mgaya. Huyu alikuwa ni mmoja wa
waliopata ajali pamoja na marehemu Mtikila.
Ikumbukwe kuwa Magaya ni mmoja wa mashabiki
muhimu sana wa Mgombea Urais kupitia Ukawa
ndg Edward Lowassa.Taarifa za siri zinasema kuwa
Mchungaji Mgaya na Mchungaji Mtikila walikutana
takribani mwezi mmoja uliopita tu na kwamba kuna
wasiwasi kuwa alipewa kazi maaluum ya
kuhahakisha amamuua Mtikila.
Taarifa kutoka nyumbani kwa marehemu zinasema
kuwa Mchungaji Mtikila akiwa na Mchungaji
Patrick Mgaya walianza safari siku ya Ijumaa jioni
kwenda mkoani Njombe ambapo waliambatana na
madereva wawili ambao Mchungaji Mtikila
hakuwafahamu. Aliewafahamu watu hawa wote ni
Mchungaji Magaya ambae ndie aliekodisha gari
waliokwenda nayo Njombe kupitia kwa Ndg Victor
James Manyii ambaye mbali ya kutoa gari
aliyokodisha pia alitoa madereva wawili ambao
pamoja na Mchungaji Mgaya wao hawakufa
isipokuwa Mchungaji Mtikila pekee.
Ajali hii imeacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa
mfano ukiangalia shingo ya marehemu Mtikila
utaona kuna kitu kama kamba ambayo inaweza
kuleta tafsiri kuwa ilitumika kumnyonga marehemu.
Pili, kwanini mwili wa marehemu hauna hata kovu
wala mchirizi wowote wa damu? Je, ni nani
alimpiga picha Marehemu Mtikila? Je, Patrick
Mgaya ni nani? Kabla kuwa mchungaji alikuwa
anafanyakazi gani? Je gari lile lilipinduka lenyewe
au liligongwa? Na kama lilipinduka ni kwanini
liharibike eneo la mbele pekee?Je Ni chombo gani
kilikuwa cha kwanza kumpiga picha na kusambaza
kwenye mitandao?
Patrick Mgaya alipopiga simu nyumbani kwa
marehemu alisema wamepata ajali na kwamba
kulikuwa na majeruhi wengi sana akamaliza kwa
kusema mtuombee kisha akakata simu, je, hao
majeruhi wengi ni akina nani? Vyombo vyetu vya
Ulinzi na Usalama muhojini Mchungaji Patrick
Mgaya maana zipo dalili kuwa kuna mengi
anayoyafahamu kuhusu tukio hili. Pia fuatilieni
uhusiano uliopo kati ya Rais Paul Kagame, Patrick
Mgaya na EADWARD LOWASSA. Pia nashauri Jeshi
la Polisi kumuhoji mtu anaeitwa Dr. Jean Bosco
Ngendahimana ambae anaishi nyumbani kwa
marehemu pale Mikocheni.
Wale wote wenye misimo thabiti juu ya kuchukia
Rushwa na Ufisadi wachukue tahadhari. Nasema
hivyo sababu Humphrey Polepole alivamiwa
nyumbani kwake Mbezi na Dkt. SLAA anapokea sms za vitisho
Connect With Us