Tanzania, Tanzania.. nchi yenye mali nyingi.........., watu wengi wa ulaya wanaililia sana......Huu ni moja ya wimbo tulioimba kipindi cha mwalimu.

.....Ninapokwenda safarini, kutazama maajabu, biashara nayo makazi,sitaweza kusahau mimi mambo mema yakwetu kabisa,Tanzania Tanzani....nakupenda kwa moyo wote....

...yakwanza ni Serengeti Ngorongoro Manyara na Mikumi oooh Tanzania hoye......

Hizi ndizo nyimbo za pekee za kuithaminisha Tanzania...

Leo hii najiuliza ipo wapi dhana ya nchi yenye mali nyingi huku wakazi wake wakiachiwa mahandaki, ni hatari sana endapo yule aliyesema ngoja Watanzania wasome akitokeza leo ..nahisi atajuta sana na kuionea huruma Tanzania yeke kwani si ile aliyoiandaa kuwa.

Ipo wapi dhana ya mambo mema yakwetu kabisa...tumezama tukaibukia katika mfumo wa mimi kwanza.

Hii ni Serikali sikivu, hakika Serikali inayosubiri kuambiwa ili isikie..wengine wakasema ati kipofu...haoni husubiri kuambiwa tu....hayo ni yao si ya mimi.

Leo najitokeza kumulikia swala la Serikali kutelekeza WAZEE.

Ndio, ukitembelea nchi mbalimbali duniani utapata mifumo mizuri na mazingira mazuri ya kuwahifadhi wazee kutambua mchango wao wa ujana wao kulifikisha taifa pale lilipo.

Kinyume na Tanzania,nimesikitishwa sana na kitendo cha Serikali kuwafanya WAZEE KUWA WASAFISHA NJIA ZA LAMI MIJINI.Takribani nimetembea mikoa mingi sana nchini kama si yote na kila mkoa ninaopita nimejaribu kuangalia wasafisha njia yaani wale wanaoondoa mchanga barabarani nikatambua idadi yao kubwa ni WAZEE.

Naiuliza Serikali, Hawa wazee wamewakosea nini hata kuagiza halmashauri zifanye ajira ya kusafisha barabara za lami ziwe mahususi kwa WAZEE..

Ni kweli , wazee wakati mwengine wanamahitaji yao , ndio Serikali imeshindwa kukidhi mahitaji yao ni sawa pia..Lakini ni vipi kuwaharakishia vifo WAZEE kwakuwaajiri kufanya kazi yenye vumbi jingi na katika mzingira magumu kiasi hiki.Ukizingatia WAZEE viungo vyao vya mwili tayari havina uimara wakukabiliana na mazingira magumu.

Haya basi tuseme WAZEE nao wanapaswa wajishughulishe..ni sawa kwa mtazamo wenu..sasa ni vipi kuwawekea mazingira salama ya kazi.Hata vizuia vumbi vyakuweka puani hamna,jamani..

Tukumbuke hawa wazee wa leo ndio walioiandaa Tanzania ya leo na ninyi kuwa hivyo mlivyo.Bila juhudi za wao huenda hata Tanzania isingekuwa kama ilivyo sasa.Si maanishi WAZEE wakae tu wasifanye kazi endapo wanauwezo wakufanya kazi bali.....

Ni ombi langu na rai yangu kwa Serikali iliyopo madarakani kabla haijaondoka ilimulikie hili.Muwawekee WAZEE mazingira mazuri ya maisha na endapo mmeona ni vyema wajishughilishe basi muwaandalie mazingira bora ya kazi vilevile niiombe Serikali kuagiza kusitishwa kwa ajira za WAZEE wasafisha njia.

Na huku ndiko kuimba mambo mema yakwetu kabisa..ndipo uhalali wakuimba nchi yenye mali nyingi kwa maslahi ya watu na vizazi vyake.