Bibi kizee mmoja amenyongwa hadi kufa na wanakijiji wenzake kwa tuhuma za ushirikina, kaskazini mashariki mwa India.
Polisi katika jimbo la Assam wamesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 63, amekuwa akilaumiwa kusababisha magonjwa katika eneo la wakazi hao.
Watu saba wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo.
Polisi nchini humo wamesema karibu watu 90, wengi wao wanawake wamenyongwa, kuchomwa moto wakiwa wazima au kuchomwa visu hadi kufa baada ya kudaiwa kuwa ni wachawi katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Imani za kishirikina zinaaminika kushamiri miongoni mwa makabila katika jimbo hilo.