Niwape pole sana Mh. Kinana na Nape kwa jitihada zao. Kwa upepo unavyovuma sasa ni wazi hakuna njia mbadala. Jiandaeni kukabidhi mamlaka kwa Amani name Usalama. Kila mbinu yenu inateleza. Gharama za kukodi Viti na malori kuwasomba wananchi kuhudhuhuria mikutano yenu mwamdanganya nani? Kwa nini kututia aibu kenda kuazima hata BVR Kenya na Nigeria. Fedha za migodi mnapeleka wapi? Si mnatamba uchumi unakua kwa asilimia saba.? Naomba chonde chonde muwatumie jamaa wa TISS wawajulishe huku mtaani tunawaonaje na sasa tumeshaamua kuwamwaga Oktoba 2015.