Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  254
  Rep Power
  7
  Likes Received
  17
  Likes Given
  0

  KUSAMBAZA NAKALA CHACHE ZA KATIBA PENDEKEZWA NI MKAKATI WA USHINDI?

  Kwa nini wenye dhamana wanaendelea kufanya makosa ya dhahirI kila hatua waifanyayo? Kama kweli Katiba hiyo imebeba maoni ya wananchi kwa nini zitolewe nakala chache?

  Tutaipitishaje wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi pamoja na mmoja wa Kamati muhimu wakati wa BMK wamefikishwa kwenye Baraza la Viongozi kwa tuhuma za kukosa Maadili kwa viongozi wa UMMA.

  WAHENGA WALISHASEMA KILA MPANDA KWA HILA ATAVUNA KWA HILA, HARAMU HAIWEZI KUZAA HALALI HATA SIKU MOJA. NURU NA GIZA HAVIWEZI KUKAA PAMOJA, Ndio Maana usiku upo na giza lake hutoweka Alfajiri na mapema. Ambacho kinatakiwa ni Kukaa pamoja kama Taifa na kusonga mbele. Awamu nne za utaala wa nchi hii zitoshe kutupatia fursa ya kujua wapi tukotoka wapi tulipo na wapi tuendako.

  Tuvute kumbukumbu zetu kuona namna ambavyo BMK liliendeshwa, watu waliokuwemo, hoja zilizowekwa mezani, UKAWA walivyoondoka na Kura zilivyopigwa na hatimaye Kuserebuka kwa waliokuwemo. Ukimya kwa watanzania pengine waweza kumaanisha mshindo Mkuu.

  Sasa tunashuhudia vuta nikuvute ya Daftari la Wapiga Kura dhidi ya Tarehe ya Kura ya Maoni. Kisheria ni nani wa Kutangaza Tarehe Rasmi ya Kupiga Kura, Elimu ya Katiba na Upigaji wa Kura. Kwa nini sasa hata hakuna hofu, woga wala aibu ya kuogopa kuvunja taratibu na sheria wazi wazi? Je Historia imesimama haitatuandika vinginevyo?

  TAFAKARI

 2. #2
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: KUSAMBAZA NAKALA CHACHE ZA KATIBA PENDEKEZWA NI MKAKATI WA USHINDI?

  Nilimsikia yule mama waziri akijitapa wamesambaza tayazi nakala 1M kwa ujasiri kabisa akiongeza wanatarajia kuongeza zengine 1M basi, akaulizwa Watanzania 45M ukifanya uchanganuzi wa watoto na watu wazima, Je mnafikiri mmelitendea haki jambo hili la muhimu kabisa ?

  aaa, unajua ndugu mtangazaji , unafahamu......dededededededededdedededdededdde .....

  !!! hovyo kabisa !!!

  eti na yeye anatumaini la kuwa Rais wa Tanzania kwa akili kama hizo, yule mwenzake na spika.... ama kweli nchi hii Tanzania imegeuzwa shamba la bibi

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  390
  Rep Power
  7
  Likes Received
  16
  Likes Given
  7

  Re: KUSAMBAZA NAKALA CHACHE ZA KATIBA PENDEKEZWA NI MKAKATI WA USHINDI?

  Asha-Rose Migiro hafai urais. Kibaraka turn Hugo nae.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •