Mnyika awasilisha hoja kupinga kura ya maoni NA ELIZABETH ZAYA
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, amewasilisha taarifa kwa Katibu wa Bunge akitaka Bunge lijadili udhaifu wa katiba inayopendekezwa na kupitisha azimio la kuahirishwa kufanyikakwa kura ya maoni ya wananchi kuamua ama kuikubali au kuikataa katiba hiyo.
Pia amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza kufutatangazo laserikali la kufanyikakwa kura hiyo mwishoni mwaAprili, mwaka huu, hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Akizungumzanawaandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mnyikaalisema kama ambavyo Rais Kikwete alitumia sheria kutangaza upigaji kura hiyo, ni vema pia akafanya hivyo kuutenguakwa kuwa kuna udhaifu katika mchakato mzima.
Alisema zimebaki siku chache kufanyika mchakato huo, lakini hadi sasaelimu kuhusiana na suala hilo haijatolewakwa wananchi.
“Kwa kuheshimu sheria,Rais ajitokeze atoe tangazo la kulifuta tangazo la serikali la kufanyika kwa kura yamaoni hadi baadaya uchaguzi mkuu. La sivyo, tutakwenda kubanana na udhaifu wa utendaji wake utaanikwa bungeni,” alisemaMnyika.
Alisema kabla yamchakato huo, serikali ilipaswa kutoaelimu kwa ummamiezi miwili na kutenga siku 30 kwa ajili ya kampeni,lakini vitu hivyo havijafanyika.
“Sheria inataka kuwe na uandikishaji, utoaji elimu, kampeni na uhakiki wa walioandikishwa katika daftari kama ni sahihi au umechakachuliwa, vitu ambavyo havijafanyika mpaka sasa,”alisema Mnyika.
Aliongeza: “Rais anakiuka sheria ya nchi kwa kulazimisha kura ya maoni kufanyikaAprili wakati bado kuna udhaifu mkubwa katika mchakato mzima wa zoezi hilo.”
Aliunga mkono kauli ya aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko yaKatiba, Jaji Joseph Warioba, aliyoitoa wakati akifanya mahojiano na NIPASHE juzi.
Jaji Wariobaalisema kuraya maoni haiwezi kufanikiwakutokana na maandalizi hafifu.
Alisema kwa mujibu washeria namba tatu ya mwaka 2014, ambayo inahusu kura ya maoni, jambo la kwanzalinalotakiwakufanyika ni uboreshaji wadaftari lawapigakura, elimu kwa umma kwa kipindi cha miezi miwili kisha kampeni za mwezi mmoja.
Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza ratiba kamili ya kila eneo au uboreshaji wadaftari lawapigakura ndani ya wiki hii.
Alisema uboreshaji wa daftari hilo, ambao ulitakiwakuwahi kwa ajili yakufanikisha zoezi la upigaji kura ya maoni, lakini nalo limecheleweshwa kwa kuishia kuahirishwa mara kwa mara.
Wengine, ambao Mnyikaalisema wataenda kubanwa bungeni kutokana na udhaifu wa utendaji wao katika kuchelewesha zoezi hilo, ni Ofisi ya Rais, Ofisi yaWaziri Mkuu, Bunge, Wizara ya FedhanaWizara ya Katiba na Sheria.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alipotafuta kuzungumzia kama amepokea taarifa ya Mnyika, alisemaalikuwa katika kamati za Bunge zinazoendelea jijini Dar es Salaam, hivyo hakuwapo ofisini.
Alisema kama taarifahiyo imepelekwaofisini kwake anaamini imepokelewa na itafanyiwa kazi.
Rais Kikwete alitangaza zoezi lakura ya maoni Novemba4, mwaka jana wakati akizungumza na wazee mjini Dodoma.
Alisema sheria yakura ya maoni imeainisha mudawa wadau wa katiba kutoa elimu na kufanyakampeni, hivyo akatakasheria hiyo izingatiwe na kuheshimiwaili kuepuka ugomvi.
Rais Kikwete alisema upigaji wa kuraya maoni kuhusu katiba hiyo utafanyikaAprili 30, baada ya elimu na kampeni juu ya kura hiyo kuanza rasmi Machi 30nakuhitimishwa Aprili 29, mwaka huu kamasheria ya kuraya maoni inavyoelekeza.
Alisema imezoeleka kampeni ni siku 60, lakini baada ya kushauriana na wanasheria ilionekana siyo lazimaisipokuwa inaamuliwa na rais kwamujibu wa sheria.
MY TAKE
SIJAWAHI KUSIKIA HOJA ZA MNYIKA KUKUBALIWA KUSOMWA TOFAUTI NA WABUNGE WENGINE WA UPINZANI KAMA KAFULILA
Connect With Us