Close

Results 1 to 5 of 5
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  254
  Rep Power
  7
  Likes Received
  17
  Likes Given
  0

  RE: INGEKUWA NIMO KWENYE WATUHUMIWA NISINGESUBIRI MJADALA

  Kwa nini viongozi wetu wanasubiri majadiliano wakati iko wazi hata kwenye Imani za Mwana TANU, '' Cheo ni dhamana" Kama kweli bado wamebakiwa na element ya utu hawa jamaa wasingesubiri majadiliano. Wao waamue moja tu kupisha wengine, Mboma waliojihuzulu kwenye Operation Tokomezawameshazoea?

  Jamani tulitendee taifa letu mema. Kaeni kando wapisheni wengine mbona tumejijengea heshima kuba duniani mpka tumewaleta akiana Xi Ping, Obama, Bush na sasa tunapanga kumleta hata Putin? Tuweke Legacy yetu kwamba tumejitahidi lakini hapo ndo uwezo wetu ulipoishia.

 2. #2
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: INGEKUWA NIMO KWENYE WATUHUMIWA NISINGESUBIRI MJADALA

  Binafsi napendekeza pamoja na adhabu zote zitakazo wapata, basi kama watabaki hai watimuliwe Tanzania milele wasikanyage ardhi ya Tanzania kwani hawamthamini mzazi wao Tanzania aliye walea hata akawakuza na wengine wakaheshimika kwenda kutumikia umoja wa mataifa kwa malezi bora ya mzazi Tanzania kisha leo wamesahau na kumuhaini.

  Watimuliwe Tanzania milele wasikanyage ardhi ya Tanzania hata maiti zao zisizikwe kwenye ardhi ya Tanzania pindi wakifa kwani miili yao itakuwa laana kwa ardhi ya Tanzania hata ikasababisha maafa na majanga kwa Tanzania kwa walilomtenda Tanzania.

 3. #3
  Senior Member Mgagaa Na Upwa's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  247
  Rep Power
  6
  Likes Received
  27
  Likes Given
  22

  Re: INGEKUWA NIMO KWENYE WATUHUMIWA NISINGESUBIRI MJADALA

  Kale kausemi kao kangine "NITASEMA UKWELI, FITNA KWANGU MWIKO"
  "Kuchagua CCM ifikapo Octoba 2015, ni kukubali Katiba iliyohaririwa na Joka Mjanja Andrew Macho Makengeza Chenge Msaka Pesa ikutawale kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 ijayo.

 4. #4
  TUA
  TUA is offline
  Senior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  677
  Rep Power
  6
  Likes Received
  32
  Likes Given
  0

  Re: INGEKUWA NIMO KWENYE WATUHUMIWA NISINGESUBIRI MJADALA

  Naomba niulize mwenye jibu anijibu: Hawa jamaa kwani hata wakijiuzulu watarudisha hizo hela? Mbona wengine wameshazitumia zimebaki kidogo tu? Kuna mmoja kwenye mawio anasema yeye tuela tudogo alizopewa na RUGE ameshatumia tumia tumebaki tudogo tu. (Mawio ya jana): Hata wakijiuzulu hao mafisadi ya CCM si tutaachiwa hilo zigo tu watanzania? Kama wangejiuzulu na kuchukuliwa hatua ningeelewa angalau.
  Mimi najua kama umeibiwa ukamkimbiza mwizi hatimaye ukamkamata, cha kwanza unachomwabia ni "nipe pesa zangu" akisha kupa mnaanza kesi ya msingi je hiyo ipo kwenye hili sakata?

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Nov 2014
  Posts
  3
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: INGEKUWA NIMO KWENYE WATUHUMIWA NISINGESUBIRI MJADALA

  Tanzania ni nchi nzuri kutokana na rasilimali zetu, ingeweza kubadilika ki uchumi kutokana na kuwavutia wageni ki uwekezaji, lakini kwa ESCROW na mengine ya kifisadi tutabaki kulia na umasikini wetu.

  serikali inatakiwa kwa kila atakayebainika afilisiwe!! ushahidi uliokusanywa utumike kupitisha adhabu na siyo kuensesha kesi.
  wanyongwe!!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •