Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Senior Member Malaria Sugu's Avatar
  Join Date
  Dec 2013
  Location
  Mujini
  Posts
  2,295
  Rep Power
  9
  Likes Received
  169
  Likes Given
  29

  KUTANA NA MDADA ALIYEWAFUNIKA WANAUME UDSM

  .Ni binti,apiga A32,B+ Sita katika masomo 38,
  .Amesoma shule za kawaida za serikali
  Ni Doreen Kabuche (22), Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014,
  Amepata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science).
  Amepata alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano, hivyo kupata shahada ya kwanza daraja la kwanza.
  Amehitimu shahada hiyo akiwa miongoni mwa wanafunzi 28 wa darasa lake, lakini akihitimu sambamba na wanafunzi wengine 5,745, wanawake wakiwa ni 2,298 wa shahada ya kwanza.
  Shahada hiyo inayotolewa katika Shule ya Sayansi ya Asili (CoNaS) chuoni hapo, ni miongoni mwa taaluma adimu nchini. Ilianza kufundishwa chuoni hapo mwaka 2011.
  ALIKOTOKA
  Hajawahi kusoma katika shule zinazotoza ada kubwa za mamilioni ya fedha na badala yake amesoma shule ya msingi Mlimani iliyopo Chuo Kikuu Dar es Salaam, kidato cha kwanza hadi cha nne amesoma katika sekondari ya Forodhani na kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Benjamin Mkapa. Kote huko usafiri wake siku zote ilikuwa ni daladala.
  “Sikuwahi ku-dodge (kukacha) kipindi, sikuwahi pia kukosa discussion na wenzangu bila sababu ya maana. Na siku moja moja za mwisho wa wiki tulikuwa tukienda ku-refresh mind na wenzangu, hasa maeneo ya viwanja vya Sinza na siku nyingine Mlimani City. Ila kila Jumapili ni lazima kwenda kanisani pale chuo au kanisa la nyumbani kwetu Kigogo Luhanga,” alisema Doreen.
  “Kila Jumapili huwa sikosi kwenda kwenye ibada katika kanisa letu la Kigogo Luhanga. Vilevile mimi ni mpenzi wa muziki kama wa bendi ya Wazee wa Ngwasuma (FM Academia), bongofleva na filamu pia huwa ninazitama... (filamu) ninayoipenda inaitwa Think Like a Man, Act Like a Woman,” alisema Doreen.


  Siasa sio Ugomvi, Siasa ni hoja

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  145
  Rep Power
  6
  Likes Received
  8
  Likes Given
  0

  Re: KUTANA NA MDADA ALIYEWAFUNIKA WANAUME UDSM

  -HONGERA ZAKE, AMEDHIHIRISHA KWAMBA KILA MTU ANA AKILI SHIDA NI MATUMIZI

 3. #3
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: KUTANA NA MDADA ALIYEWAFUNIKA WANAUME UDSM

  mmmh, mi hata hongera sitoi, maksi za mlimani sikuhizi, mmm we acha tu, malekchara wana..............ni sheeeeda.

  Ila sema nini, haya mambo ya A sijui B katika soko la ajira hayamati saaana kivile wanachoangalia ni uwezo wa muhusiaka kufanya kazi mbele uzuri wa cheti kesho.Halafu ukikutana na watoto wa kariakoo wanakwambia maisha hayana fyomula ndio wanajivuni bhakhresa elimu ndogo pesa mingi tena wanakuuliza nieleze prof; yupi anatajwa kunusanusa kusemekana yupo kwa kundi la mataji Tanzania ukiachia mbali ufisadi ?

  Wanahitimisha kwakukueleza masomo ni mazingira kwa wakati huo wa kisomo ndio maana hakuwa Tanzania One pindi akiwa kidato cha 6, na wle waitwao ma TO chuoni ndio huongoza kwakudisco.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •