Close

Results 1 to 6 of 6
Like Tree1Likes
 • 1 Post By Mgagaa Na Upwa

Thread: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

 1. #1
  Senior Member Tanzania Nchi Yetu Sote's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  596
  Rep Power
  7
  Likes Received
  34
  Likes Given
  6

  TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  KAMA UTAFITI WA TWAWEZA NI WA KWELI, BASI LOWASSA HAFAI KUWA RAIS!

  Ndugu zangu,
  Kusoma ni kuzuri sana ILA kusoma ukaelewa ni kuzuri zaidi. Taasisi ya Twaweza imeleta "matokeo" ya utafiti wa "watu wao" waliowahoji kuhusu mwelekeo wa uongozi mwaka 2015. Pamoja na kwamba Twaweza wamesahau kwamba walikuwa wanawahoji watu (na siyo mawe yasiyoweza kubadilika) nimefurahi kwamba wameleta jambo ambalo wasioelewa QUALITATIVE RESEARCH hawawezi kuling'amua.

  Twende taratibu kwenye sampuli yao.

  Walihojiwa ni watu 1,445 TU. Kati ya hao, watu 482 hawakumchagua mtu yeyote (yaani hawajaamua wampe nani kura zao-na hawa kwenye andishi hili ndio watu muhimu sana (kwa sasa walioonekana kuongoza na kufuatia wanategemea maamuzi ya kundi hili)! Kama watu 482 (33% ya wahojiwa) hawamjui na hawana mpango wa kumpigia kura LOWASSA (the dreamed Twaweza's President) naona giza mbele ya Lowassa!

  Kwa hiyo 1,445-482=963

  Maana yake ni kwamba, Lowassa alipata kura 125 (13%) ya 963 na ni (8.6%) ya kura 1,445. Lakini wakati huo huo, Mizengo Pinda kapata kura 116 (12%), Samwel Sitta kura 48 (5%), Membe 39 (4%). Hii inaonesha kwamba kura 116 (Pinda) + kura 48 (Sitta) + kura 39 (Membe)=203

  Ni rahisi sana mfuasi wa Sitta+Membe (i.e Paul Makonda) kumpigia kura Pinda badala ya Lowassa. Ni rahisi sana Samwel Sitta kumpigia kura Slaa na siyo Lowassa!

  Mwisho nimalizie kwa mshangao wa kulazimishwa-Twaweza
  walikuwa wakifanya utafiti kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JMT ni Tanganyika na Zanzibar, sikuelewa kwa nini hawakwenda Zanzibar! Labda kama walikuwa wanakubaliana na Katiba pendekezwa kwamba Tanganyika ndiyo Muungano wenyewe!
  KARIBU.
  Usione niko kimya nakusubiri uropoke

 2. #2
  Senior Member Mgagaa Na Upwa's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  247
  Rep Power
  6
  Likes Received
  27
  Likes Given
  22

  Re: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  KAMA TWAWEZA WAMEWEZA KUTIKISA VYOMBO VYA HABARI KWA KUHOJI WATU 1445 BASI TUNA SHIDA?
  KISIKI likes this.

 3. #3
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  Fisadi Lowasa ana mbinu za kitoto sana, na urais atausikia kwenye bomba tu.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  9
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Re: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  Kwa hili nakubaliana na KISIKI

  - - - Updated - - -

  Tanzania Nchi Yeru Sote umefanya uchambuzi ukiwa umetulia sana

 5. #5
  Senior Member
  Join Date
  May 2014
  Posts
  431
  Rep Power
  6
  Likes Received
  34
  Likes Given
  24

  Re: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  SI KILA TAARIFA TUTAKUBALI KUMEZA PASIPO TAHADHARI KAMA HII YA UTAFITI KUHUSU LOWASA KUKUBALIKA ZAIDI NK.....!!

  UKWELI WA HALI YA KISIASA, PROPAGANDA NK KTK NCHI NA WEPESI WA WANACHI KUGHILIBIWA UNAJULIKANA KWA WENYE KUJITAMBUA!!

  NI UKWELI USIOPINGIKA KWAMBA TYR UPO MFUMO ULIOSIMIKWA KUGANDAMIZA MAISHA NA NDOTO ZA HAWA HAWA WANANCHI WAKISUBIRI MIAKA NENDA RUDI KUTIMIZIWA AHADI ZA MAISHA BORA...NDOTO ZA KUFAIDI UHURU WA KWELI WALIOPIGANIA WAASISI WA TAIFA PASIPO KUTIMIZWA!!

  NDOT ZA WATU HAWA MASKINI WALIOKALIA UCHUMI HAZIWEZI KUTIMIZWA NA WATU WALE WALE HATA KAMA TAFITI MFANO WA HII YA TWAWEZA ZITAWABEBA KWA KIASI GANI!!

 6. #6
  Senior Member
  Join Date
  May 2014
  Posts
  189
  Rep Power
  6
  Likes Received
  6
  Likes Given
  0

  Re: TWAWEZA WANALIJUA HILI LAKINI?

  Pia wafanye utafiti ili taifa lijue idadi ya watanzania wanaochukia ufisadi wa Richmond

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •