Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  254
  Rep Power
  7
  Likes Received
  17
  Likes Given
  0

  RE: KIUNDWE CHOMBO HURU KUFUATILIA MIKATABA YA RASLIMALI ZETU

  Nimekuwa nafuatilia sana mwenendo wa namna raslimali zetu zinavyoporwa bila kuwepo chombo maalum ambacho kiwe ni chombo huru kufuatilia makubaliano mbalimbali ambayo serikali yetu inaingia na wawekezaji. Kwa mfano katika sekta ya madini tumekuwa tunasikia makubaliano mbalimbali amabayo serikali imeyaingia na mengi ya makubaliano hayo yamesababisha maumivu makubwa kwa wananchi walioko jirani na shughuli za wawekezaji hao na taifa kwa jumla.

  Mifano michache ni kama ifuatavyo:-
  1. Serikali yetu huingia mikataba na wawekezaji mbalimbali kwenye uchimbaji wa madini, kwenye serikali hiyohiyo vipo vyombo mbalimbali chini ya wizara ya madini mfano, NEMC, STAMICO, OSHA nk. Lakini uwepo wa vyombo hivyo bado haujaweza kuwawajibisha wawekezaji wanapokiuka kanuni za mazingira kama ilivyotokea Nyamongo Tarime, Geita na huko Chunya Mbeya.
  2. Wananchi wa vijiji vilivyoko MBINGA kwenye machimbo ya Makaa ya mawe hsa wakazi wa Mtunduwalo, hawajalipwa fidia lakini mwekezaji anaendela kuchimba makaa ya mawe bila kutimiza masharti ya kimazingira, makazi ya wanavijiji hao yako kwenye hatari kubwa kutokana na vumbi lenye uchafu wa makaa ya mawe.
  3. Ikumbukwe kwamba kwenye miaka ya 2007 -2010 timu ya viongozi wa dini waliibuka na kuanza kufuatilia mienendo ya wawekezaji hasa kanda ya ziwa. Tuliona mambo mengi yaliyoibuliwa na viongozi hao wa kiroho. Kitu cha kushangaza ni namna ambavyo viongozi hao walivyonyamazishwa na wala hatusikii tena vilio vya watanzania wenzetu kwenye maeneo ya migodi.
  4. Tuliambiwa kwamba Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Barick inafunga mgodi wa Tulawaka, je ni faida gani iliyopatikana kutokana na uchimbaji huo wa dhahabu ya Tulawaka? Niliwahi kuona picha za mashimo yalioachwa na kutelekezwa kule Buhemba Mara yanatia kichefuchefu.

  Ni wakati muafaka wa kufunguka macho,
  Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name:	Buhemba Mashimo-8.jpg 
Views:	340 
Size:	29.9 KB 
ID:	680   Click image for larger version. 

Name:	Buhemba Mashimo-6.jpg 
Views:	331 
Size:	23.6 KB 
ID:	679   Click image for larger version. 

Name:	Buhemba Mashimo-9.jpg 
Views:	325 
Size:	41.7 KB 
ID:	681  

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  254
  Rep Power
  7
  Likes Received
  17
  Likes Given
  0

  Re: KIUNDWE CHOMBO HURU KUFUATILIA MIKATABA YA RASLIMALI ZETU

  Chombo hicho naomba kiwe na wadau wafuatao,
  Wasomi wetu wazalendo, wanaharakati, Viongozi wa Dini, vyombo vya habari, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wawakilishi kutoka vyama vya siasa, taasisi za elimu ya juu. Wazee wetu wazalendo wasiokuwa na tuhuma zozote.

  Wadau hawa wawe huru kabisa bila kuingiliwa na chombo chochote cha dola

 3. #3
  Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  79
  Rep Power
  6
  Likes Received
  2
  Likes Given
  0

  Re: KIUNDWE CHOMBO HURU KUFUATILIA MIKATABA YA RASLIMALI ZETU

  Yote msemayo ni kweli tena kweli tupu.
  Kupata tume huru na isiyoingiliwa ni ngumu. Ilitakiwa madaraka makubwa ya rais yapungue, ili ripoti hiyo hiyo ikabidhiwe bunge moja kwa moja.
  Rais anahusika na kila dial kubwa, hivyo ikiwa inagusa familia, marafiki au wateule wake ataizuia kwenda popote.

  Mikataba yote mikubwa ni siri kati yake na china, usa, makaburu nk, tupigane kwanza madaraka yake iondoke

 4. #4
  Senior Member Tumbo's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Location
  Tanzania
  Posts
  358
  Rep Power
  7
  Likes Received
  18
  Likes Given
  22

  Re: KIUNDWE CHOMBO HURU KUFUATILIA MIKATABA YA RASLIMALI ZETU

  Ndugu yangu Chikaka, pendekezo lako ni zuri na sahihi, kila mtu mwenye dhamira njema,mapenzi mema na uzalendo katika taifa letu Tanzania; bila shaka angependa kuona mikataba yote inayohusu rasilima za taifa ziwanufaishe watanzania wote na Taifa kwa ujumla, lakini ni bahati mbaya sana kwa mfumo wa utawala wa ccm na serikali yake hilo haliwezekani..! Kwani wengi kama si wote ndani ya serikali ya ccm ni ukoo wa panya kila mmoja anajichukulia chake mapema. Ni mwenda wazimu tu anayeweza kukataa masuala yahusuyo miiko na maadili ya viongozi wa umma, ama watawala isiingie katika katiba inayopendekezwa.
  HAKI ikitendeka, AMANI hutamalaki, hakuna AMANI pasipo HAKI.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •