Close

Results 1 to 1 of 1
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2014
  Posts
  166
  Rep Power
  6
  Likes Received
  5
  Likes Given
  9

  Cool SITAICHOMA KATIBA YA SITA, NITAITUNZA IKUMBUKWE NA VIZAZI VIJAVYO KAMA UOZO WA CCM

  Watu wengi wenye uelewa wameughadhibishwa na uharibifu mkubwa wa kodi za wananchi kwa jambo ambalo mwisho wake si mwema kwa mustakabali wa Taifa.
  Baadhi ya watu wamepania kuichoma moto katiba hiyo inayopendekezwa ili kuonyesha hisia zao juu ya utekaji wa mawazo yao, kwangu binafsi nadhani wana haki ya kuonyesha hisia zao pengine si kwa namna hiyo.
  Natamani sana kuitunza katiba hiyo katika maktaba yangu ya nyumbani japo ni jambo gumu kutokana na marafiki,jamaa na ndugu kuipinga kila kona,ndugu historia huhifadhiwa na ni jambo jema kwa minajili ya kuwakumbusha Watanzania wajao kuwa kwa wakati mmoja,watanzania wa chama kimoja kwa siku 130 walikula fedha kwa manufaa yao nakuleta hili chapisho.
  Nadhani nao watakumbukwa katika msafara ule ule wa kina chifu Mangungo wa Msovero na nk.
  wikiendi njema.!
  Last edited by Masalu; 27-09-2014 at 19:53.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •