Ilikujiepusha kukutana na mtu asiyefaa katika maisha yako ya ndoa na umpendaye hali itakayokupelekea kurudi aidha kiuchumi,kielimu,kisiasa na hata kiimani;Hivyo ni muhimu kama kijana kuwa makini na kwamba si kila mwanamke au mwanaume akupendaye afaa kuwe mke au mume.
Tuepuke hasa vijana kuokotana ilihali unahitaji mtu sahihi wakukusaidia kufanikisha malengo yako ,ni watu wengi wameingia kwenye majuto makubwa kutokana na kushindwa kupata watu sahihi kwenye maisha yao.Samahani lakini mfano halisi mh.zitto ambaye juzi hapa alianikwa na mwanadada Diva nukushi(e-mail) zake hadharani wakati ni mambo ya siri,huu ni mfano mmoja lakini iko mingi sana ambayo wewe unaifahamu vyema.
Sasa mtu sahihi wakuwa naye kwenye ndoa ni yupi?
Ni huyu hapa:
1.Mwenye maono na mikakati ya kusonga mbele si hawa mazuzu wa mjini wa bata batani.
2.Maadili eg lugha nzuri,mavazi,heshima,( muhimu bila kujali uzuri,fedha)
3.mvumilivu na mwepesi kusamehe sio kidogo tu kwetu sikuua.
4.Msiri (ni muhimu kwenye ndoa ref.zzito vs Diva)
Bila kuathiri sifa za hapo zile 6C kama car,cash,clothes nk zaweza kutumika kwa umpendaye.
Nyingine leteni mezani!!!