Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2014
  Posts
  166
  Rep Power
  6
  Likes Received
  5
  Likes Given
  9

  Raisi ajaye,Atupe katiba ya Tanganyika kabla ya ile Muungano.

  Ndugu zangu,baada ya migogoro mingi ya mchakato wa katiba mpya,ni muda wa muafaka kabisa wakusaka katiba ya Tanganyika hata kabla ya kuanza upya huu,tena hapo 2016 tuanze na katiba ya Tanganyika.
  Kwa maoni yangu, ni wazi kwamba Sisi wa Tanzania bara( Tanganyika) ndio wenye uhitaji mkubwa wa katiba kuliko zanzibar ambao wana katiba yao.mkitazama vizuri ndugu zangu sisi ndio wenye mahitaji makubwa hasa ardhi,rasilimali,mahakama kadhi, uchumi, haki za wafanyakazi,uhuru wa mahakama na nk.Lakini waasisi kwa maana ya watoa hoja hii ya kutaka katiba mpya wengi ni watu wa Tanzania bara;Hakika tunastahili kupata katiba yetu ,ndugu zangu tulitakafari hili kama huu ni muda muhimu wa nasi kuwa na katiba yetu kabla ya ile ya muungano hapo 2016.
  Hivyo basi napenda kutumia fursa hii kuhamasisha ndugu zangu kumuomba raisi ajaye atupe katiba yetu kabla hata ya ile muungano ambaye iko bungeni sasa.
  Nawasilisha!!!

 2. #2
  Senior Member Mchambawima's Avatar
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  152
  Rep Power
  7
  Likes Received
  2
  Likes Given
  1

  Re: Raisi ajaye,Atupe katiba ya Tanganyika kabla ya ile Muungano.

  Walichofanya ni kuzungukazunguka na kulichukulia swala la muundo serikali tatu kama mawazo ya UKAWA wakati ni mawazo ya wananchi wenye hekima na busara tele. Sasa kiko wapi kama siyo utoto?

  Walipokuwa wanapiga kelele za kulazimisha muundo wa serikali mbili walikuwa na lao jambo wala si gharama kama wakivyokuwa wakitoa hoja hiyo dhaifu machoni pa Watanzania. Kupata katiba yenye imara lazima kuanza na moja. Maskini pesa za walalahoi zimetafunwa hivi hivi kimchezo.

  Mimi naona kwamba kwa makamu kilichoongezeka sana ni vyeo tu, lakini hawa makMu wa rais wana majukumu yao tayari. Rais wa Zenji, mgombea mwenza na waziri mkuu.
  Kwanza serikali yao ndiyo yenye gharama kubwa:

  Kwa mfano: Mapendekezo ya Warioba: Mawaziri wawe 15. Mapendekezo yao ni mawaziri 30. Mapendekezo ya Warioba: idadi ya wabunge 75 wa muungano. Mapendekezo ya ni wabunge 360.

  "Rais wa Zanzibar atakuwa makamu wa pili wa Rais na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa tatu wa Rais huku ikitamka kwamba makamu wa kwanza wa Rais ni Mgombea Mwenza wa Rais wakati wa uchaguzi." Tanzania Bara haipukiki!

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  468
  Rep Power
  6
  Likes Received
  28
  Likes Given
  17

  Re: Raisi ajaye,Atupe katiba ya Tanganyika kabla ya ile Muungano.

  Naona wanafiki siku hizi wala hawatamki neno TANZANIA VISIWANI. Wanasema Zanzibar sasa kama
  identity ya Zanzibar ipo nainazidi kupewa mamlaka, Tanganyika ndiyo ipotee? Haiwezekani kamwe.
  Inamaana kwa ulafi wa madaraka ya watu wachache tufanye Tanganyika ya watu 44 milioni
  itawaliwe na watu millioni 3? Pamoja na Zanzibar kusema Tanganyika imevaa koti la Muungano
  lakini hakika Tanganyika inanyonywa na Zazibar kwa ubali kabisa. REJEA MCHANGO WA KEISSY Mjumbe wa
  BMK Dodoma hivi karibuni na karibu auawe na wazanzibari wakiwa Dodoma (Tanganyika) bila
  msaada wa watanganyika.
  Ndugu zangu, tuamke usingizini, sasa imeshafika jioni. Itakula kwetu nasema ikiwa hatutagundua kwamba
  tumefanywa watumwa wa ccm. Tutajitoa utumwani wenyewe kwa nguvu zetu.
  Serikali imeshafanya Tanzania kuwa ni utawala wa kijeshi usio rasmi ali mradi WASAKA TONGE/
  WACHUMIA TUMBO WA CCM WAENDELEE NA UOVU, UFISADI, RUSHWA NA UBABE WAO
  TUKATAE KWA NGUVU ZOTE

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  137
  Rep Power
  7
  Likes Received
  9
  Likes Given
  11

  Re: Raisi ajaye,Atupe katiba ya Tanganyika kabla ya ile Muungano.

  "Siku moja akatokea kiongozi wa Taifa letu, akatuambia huko nje kuna hela nyingi kuliko hapa nyumbani, mwambieni wewe ni mpumbavu" Mwalimu J.K. Nyerere.

  "Kama kuna mtu ambaye anaamini nchi hii inaweza kuendelea kwa kusaidiwa, anajidanganya, Narudiia tena, Katika nchi hii kama kuna kiongozi anaamini nchi inaweza kuendelea kwa kupewa misaada, anajidanganya" Benjamin Mkapa.

  "Unapoenda kuomba siyo kwamba wewe unapenda tu kuomba. Huko nje kuna mataifa yenye hela nyingi tu, unachotakiwa ni kujieleza, wakikuelewa, watakupa" Jakaya Kikwete.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •