Wadau, poleni kwa majukumu ya kila siku; Leo katika safari zangu wilayani Korogwe katika sehemu iitwayo Magoma huku milima nilikutana na mashamba makubwa ya bangi huku ikiwa imezungwa na migomba na miti.
Kitu kilichonishangaza ni baadhi ya viongozi wa vitongoji kujua hali hiyo bila kuchukua hatua; Wafanyabiashara ya bangi ambao wengi nikutoka Dar -es-salaam ambao huagiza bangi kutoka milimani huku kwenye mashamba.
Kiukweli nilitaka kujua zaidi ni nani wako nyuma ya sera hii ya kilimo kwanza? Hapo ndipo nilipobaini baadhi ya polisi korogwe mjini ni wahusika,wafanyabiashara fulani hapa mjini dar!!
Kilio changu: Jeshi la polisi livunjwe halina msaada kwa jamii!!, mkuu wa wilaya ya Korogwe chukua za haraka dhidi ya viongozi vijiji. na mwisho elimu ya madhara ya madawa ya kilevya itolewe.
Wadau, samahani sana sikuweza kuchukua picha kwasababu simu ilizima hivyo sikupata picha ya uozo huu.