Close

Results 1 to 3 of 3
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jul 2014
  Posts
  166
  Rep Power
  6
  Likes Received
  5
  Likes Given
  9

  Kwanini tunajua siri za mafanikio lakini hatufanikiwi?

  Asilimia kubwa ya vijana na hata wazee mara zote huwa na uwezo mkubwa wa kueleza mbinu mbalimbali ambazo hudhaniwa kuwa ukizitumia waweza fanikiwa lakini hao hao utashangaa maisha yao.
  Wakati mwengine waweza jiuliza ni kwanini ma profesa wa marekani ambao baadhi yao na ma profesa wetu waliketi darasa moja huko ughaibuni lakini hawa kwetu hoi? Lakini pia dunia hivi leo kuna utitiri wa vitabu vya kutoa elimu juu kufanikiwa kwenye jambo fulani aidha elimu, uchumi, ujasiriamali,biashara nk ambavyo watu wengi dunia huvisoma lakini wapi? .
  Nawasihi wachangiaji mnipe mawazo yenu juu ya hili, watafiti wanasemaje? je ni hulka ya binadamu kuwa hivyo? wanasaikolojia tuambieni?
  Najua mbinu za kuwa tajiri lakini siwi,mbinu za kufaulu mitihani lakini bado watu wanafeli? njia ya kumpendeza mungu ,watu wanazijua lakini wapi? Nini hasa tatizo binadamu huzaliwa hivyo?
  Nimechokoza mada, " Kwanini tunajua mbinu au siri za mafanikio lakini hatufanikiwi? nipe wazo!!
  wikiendi njema!!!

 2. #2
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: Kwanini tunajua siri za mafanikio lakini hatufanikiwi?

  Kuna tafauti kubwakati ya mawazo na utekelezaji, wengi tunawaza na tunamawazo ya juu sana, tukirejea katika utekelezaji utapata ni wepesi wakukata tamaa, na wengine hata yaletuyawazayo hubaki kwa vichwa, implimintation=o, huku tukitanguliwa sana na mtazamo hasi wakutanguliza kushindwa hata hatua za mwanzo kabisa la wazo.Utasikia, kweli nitaweza? mmmh, hapana bora ni................

  Lingine pia ni Mazingira anayokulia muhusika, huchangia kwa asilimia zaidi ya 60 katika mafanikio ya muhusika.Mfano, umekulia kijijini huko ndani kabisa, gari kuliona ni basi tena linapita jumapili mara moja kwa siku.Kwa muhusika wa namna hii , ni vigumu kwake kufikiri anauwezo wa kununua gari bali atabaki kutambua gari ni kwa wateule toka mbinguni, hata siku akipata kama bado akili inabaki na mazingira yaleyale ni wachache wetu wanaoweza kubadilika.

  Watu wanaokuzunguka pia huchangia kwakiasi katika mafanikio ya muhusika.Ndio utapata imeandikwa mwenye nacho atazidi kuongezewa, ukipata ukoo wa watu wenye mshikamano umoja na upendo sambamba na mafanikio, ukiwa katika hii jamii basi utapata mafanikio fulani kwani changamoto toka kwao zitakufunza jambo.Mbona kaka kaweza na nimeshuhudia haya machoni mwangu wala si miujiza, kwanini mimi ? ngoja nipambane na mimi kulinda heshima yangu.

  Kujitambu ni sehemu ya mafanikio, wapiulipotoka, wapiulipo wapi unaenda, ni mambo ambayo yananafasi yakumsaidia muhusika katika safari ya mafanikio.Utapatakijana unamuuliza, kwa mwaka uliopita kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa 12, ni kiasi gani cha fedha kimepita mikononi mwako? kiasi gani ulitengeneza kwa juhudi zako? na ni nini matumizi ya hizo ? na mwaka huu unatarajia kukuza vipi kipato kuzidi mwaka jana ? utapata hola.Tunabahatisha tu.

  Lingine ni tafsiri ya mafanikio, kwangu mimi mafnikio si kuwa na gari zuri, ghorofa, fedha nyingi na releated issues in money.Kwangu mimi mafanikio niweze kumudu mahitaji ya msingi vhakula, malazi na mavazi kiuhakia, hilo ni moja lingine ni FURAHA , AMANI NA UPENDO.Kwani hata niwe na magari mengi, ghorofa ndiko niishipo lakini kama hakuna amani kwa nyumba hiyo ,upendo hapan wala furaha na gari hilo hiyo nayo ni adhabu nyingine inayochangia kumuathiri muhusika kisaikologia na kupelekea kifo.

  Ni hayo.

 3. #3
  Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  97
  Rep Power
  7
  Likes Received
  4
  Likes Given
  4

  Re: Kwanini tunajua siri za mafanikio lakini hatufanikiwi?

  Mkonge

  Siri ya mafanikio inaendana na kipimo cha mafanikio. Hivyo basi, kujua siri ya mafanikio ni suala moja na kupima mafanikio ni suala tofauti. Namna gani unaunganisha mawili haya ndio utakuwa na fursa nzuri kufahamu kama umefanikiwa ama lah!

  Wakatabahu

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •