Habari wana MF ,natumai mko njema .
Nije kwenye mada hapo juu,nina hakika hasa wakristo wanamjua vizuri nabii Eliya ambaye alipambana vema na mfalme dhalimu Ahabu.Eliya nabii alichukua jukumu la kuomba kuhakikisha mvua hainyeshi katika nchi ile aliyoishi Ahabu lakini kwa bahati mbaya naye akawa mhanga wakutonyesha mvua hatimaye akaokolewa na Mungu kwenye kadhia ile,sifa moja ya eliya nikujiona bora kuliko wengine wamuabudio mungu.
Tofauti kidogo na nabii eliya,wako waandishi wa habari ambayo mara kwa mara kupitia vituo vya televisheni, redio pamoja magazeti walikuwa wajitenga dhidi ya maovu ya polisi dhidi ya waandishi wakidhani kwamba wao hayatowakuta au wao ni tabaka jingine la waandishi.Kwa mfano ukiwasikiliza waandishi vituo vikuu fulani kuhusu ukandamizaji wa polisi dhidi ya waandishi watakwambia ni " makanjanja wa waache waadhibiwe" hivyo kwao si habari.lakini je vipi mwandishi wao akisanyanyaswa na polisi au hata kuuawa?; Huwezi kuamini hata habari za leo kuhusu kushambuliwa ziko kibaguzi baadhi ya magazeti yameandika hivi "Baadhi ya waandishi washambuliwa" ni ile ile kauli ya kujihisi huhusiki na wale wahanga ni wakorofi sio watii.
Wakati tunamlilia mwangosi,waandishi fulani na magazeti yao na wengine mitandaoni wakasema " Mwangosi alijidai anajua kutafuta taarifa, amekipata" Tukasema haya, je kibanda!? nae eti mkorofi eeh!! kubenea? aaah hao ndio majasusi!!.
Ile dhana ya baadhi ya waandishi kijiona bora kuliko wengine labda kutoka na mikono ya wakuu,ni kama nabii Eliya aliyemwambia Mungu " Nimesalia mimi pekee nabii wako" lakini Mungu akamjibu " Nimesaziwa watu7000 ambao wananipenda" Wazi sasa kwamba waandishi wapinge kwa pamoja kwa nguvu zote ukandamizaji mkubwa wa jeshi la polisi badala kutengana,la sivyo mtakwisha ukizingatia uchaguzi ni mwakani 2015 ref( pitia ripoti ya ujerumani), pili zingatieni uadilifu hio ndio nguvu yenu badala ya wakuu (ref. kauli ya werema" Tanzania hakuna magazeti ni vipeperushi).
Mwisho yaliojili jana dhidi ya waandishi, akina Eneck bwigune tujifunze kwa pamoja !!! Tutakwisha