Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member Tanzania Nchi Yetu Sote's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  596
  Rep Power
  7
  Likes Received
  34
  Likes Given
  6

  MAISHA YA NDOA NA MICHEPUKO YAHITAJI UVUMILIVU MKUBWA

  Kijana mmoja alioa mke ampendaye sana kwa harusi ya kifahari iliyoacha gumzo mtaa mzima
  Baada ya kuishi kwa miaka kadhaa ya ndoa siku moja kijana akagundua kuwa mke wake anatoka nje ya ndoa na hapo kijana akajaa upepo na kufata baba yake kumpa taarifa kuwa anataka kumuacha mkewe kwa sababu anatoka nje ya ndoa.
  Baada ya kijana kumueleza baba yake taarifa za mkewe na azma yake ya kumuacha,baba akamwambia mwanangu usimuache huyo mke. Kijana hakuelewa somo la baba yake na akawa king'ang'anizi akitaka kumpa talaka mkewe lakini baba alimsihi asimuache.
  Baba alipoona mwanawe anasononeka sana juu ya kitendo hicho cha mkewe,basi baba akamwambia kijana wake kuwa anataka kumpa dawa ya tukio hilo na kijana akakubalia.Baba akamwambia basi wewe ujifanye unaumwa sana halafu mimi nitasema tukupeleke kwa mganga,najua familia itakataa halafu mimi nitaenda mwenyewe kwa mganga kuchukua dawa ya tatizo lako.
  Basi baba na kijana wake wakakubaliana na kijana akaanza kujifanya anaumwa sana,baba yake akapendekeza apelekwe kwa mganga.Ndugu wa familia wakakataa katakata na hapo baba akaondoka kwa hasira kuwa anakwenda kwa mganga kuchukua dawa.
  Baba akaondoka na kwenda alikokujua kisha akarudi na kifurushi na hapo akaanza kutoa maelekezo ya mganga juu ya kuitumia hiyo dawa.
  Maelekezo ya mganga kwa mujibu wa baba ni kuwa dawa hiyo itengenezwe na mwanamke ambaye hajawahi kutoka nje ya ndoa yake.basi hapo kila mmoja akaanza kutoka nje akianza mama wa kijana,shangazi,dada na mke wa kijana huyo.Baada ya wote kutoka baba akamgeukia kijana wake na kumwambia,unaona mwanangu hata mama yako kashindwa kukutibu sasa hapo unasemaje?Kijana hoi.
  Usione niko kimya nakusubiri uropoke

 2. #2
  Junior Member dismainda's Avatar
  Join Date
  Sep 2014
  Location
  mbinguni
  Posts
  9
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  2

  MAISHA YA NDOA NA MICHEPUKO YAHITAJI UVUMILIVU MKUBWA

  hhhhaaaaa nahisi wazo la talaka liliishia hapo hapoo

 3. #3
  Junior Member
  Join Date
  Nov 2014
  Posts
  3
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  MAISHA YA NDOA NA MICHEPUKO YAHITAJI UVUMILIVU MKUBWA

  hahahahahahaha, wachache sana wameshinda hilo jaribu.

 4. #4
  Junior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  3
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: MAISHA YA NDOA NA MICHEPUKO YAHITAJI UVUMILIVU MKUBWA

  Hah hah hah

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •