Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  240
  Rep Power
  7
  Likes Received
  2
  Likes Given
  2

  KATIBA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

  Hakuna kitu kizuri kama kujitambua hakuna jambo jema kama kuukubali ukweli hata kama huupendi na hakuna jambo linapendeza kama kubalika tokana na wakati na hali halisi ya kimazingira.Nchi yetu inapitia mahali pagumu sana kimazingira na hali suala la katiba mpya ya nchi hii si la kufanyia masikhara kama tufanyavyo sisi,leo naomba kuuliza kila mhusika kwa nafasi yake na maaamuzi yake juu ya suala hili,naanza na raisi kikwete hivi kweli mpaka sasa hujajua hali ikoje?kweli una nia thabiti ya kuiandika historia iliyo njema ya uongozi wako?unayoshauku ya kukumbukwa ukimaliza uongozi wako?kama majibu haya unayo yaliyosahihi basi geuka ukafanye uamuzi sahihi.pili nakuuliza mwenyekiti wa BMK ndugu sita kweli wewe unamjua MUNGU na kumuogopa?kweli unaamini huwezi jaribu kiona alichojaribu kukiona mwigulu jambazi nchemba?uzalendo wako umefia wap?mwisho nimalize na ndugu zangu ccm niulize mko tayari kuona raia tunauana?mkipata majibu kila kundi hapa lipo mtandaoni naomba mnijibu,ndugu zangu ukawa wakiendelea hivi tufanyeje?hatuwezi kuwasubiri muda wote na tuchukue hatua

 2. #2
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: KATIBA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

  Ujue hili sakata la BMK kwa walio makini watajifunza mengi sana na zaidi kuhusu siasa na wanasiasa.

  Kuna vyama nchini sasa vikishindwana kwa hoja ndani ya chama wanachama hao hao wanakuwa maadui wakubwa kwa wale walioshindwa dhidi ya washindi na kutokea mgawanyiko ama mpasuko huku washindi wakijigamba waende zao tu kwani wanatutisha nini.Wasio na hitaji la kutambua thamini na umuhimu wa UMOJA na MSHIKAMANO.

  Kuna vyama ambavyo wakishindana kwa hoja ndani ya chama na upande mmoja kushinda, wote kwa pamoja hupokea matokeo ya ushindi wa upande huo na bila kinyongo wala mpasuko na huja pamoja na kufanyia kazi tena kwa dhati matokeo hayo bila kusita sita.

  Sasa, hawa watu/vyama vya namna hii hawawezi kukaa meza moja, kwani ni sawa na huyu anatumia haramu na huyu hatumii, huyu anafahamu kucheza Taarab huyu kiduku, hizi nyimbo hazifanani midundo lazima mmoja atatoka tu kupisha.

  Tunatarajia kujifunza mengi toka kwa ujio wa BMK.

 3. #3
  Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  98
  Rep Power
  7
  Likes Received
  5
  Likes Given
  2

  Re: KATIBA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

  ndugu mpost mada hapa nataka nikujuze kuwa kikwete anajua na anatambiua mwisho wa mchakato huu na ndo maana amekaa kimya na zidi anajua mwisho wa mchakato huu ni mbaya kwa wananchi ila ameamua kukaa kimya, lakini binafsi niseme hawa viongozi wetu wanasubiriwa na mahakama ya kihalifu ICC kama wataz watauana kutokana na ukiritimba wa MACCM haya, na hata hivyo kuna wanasheria maarufu wanajiandaa kufungua kesi ya madai ya matumizi mabaya ya pesa ya umma huku wakijua hawakuwa na dhamira safi na mchakato huu. na kimsingi ccm hawa na kikwete wao wana majibu ya maswali yako.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  May 2014
  Posts
  431
  Rep Power
  7
  Likes Received
  34
  Likes Given
  24

  Unhappy Re: KATIBA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

  Pole Mgoc,

  Swali lako zuri sana lkn wala huhitaji kulielekeza kwa wengi uliowaorodhesha kama wahusika! Jibu ni raisi sana na kimsingi ulikwisha jibiwa hata kabla hujaliweka humu!

  Uliyeanza naye, raisi kikwete ndiye alfa na omega! Anajua kila kitu. Tatizo kwako na kwa wananchi walio wengi ni ukweli kwamba hajatuonyesha kuwa na nia thabiti ya kuiandika historia iliyo njema ya uongozi wake na kututendea wananchi haki!! Ukweli ni kwamba wananchi walio wengi wamekwisha kata tamaa na huyu rais! Akiamua kurekebisha mambo, ni mara moja tu anaondoka kwenye uhafidhina na ubinafsi wa kulinda maslahi ya CCM ,na badala yake anahamia kulinda na kutetea maslahi ya wengi, wananchi..huu ni muujiza tunaosubiri dakika hizi za majeruhi! Kama unasali, basi omba sana Mgoc wa Ndima, kwani Mustakabali wa Taifa uko njia panda na kwenye mashaka makubwa!

  Hawa wahafidhina wengine, akina Sitta na wengine, wala sikushauri upoteze muda nao, kwa sababu....The Buck Stops With Mr. President!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •