Uchumia tumbo ndani ya Taifa lenye utawala mbovu mithiri ya kichwa cha mwendawazimu, ni nyenzo muhimu sana inayotumiwa na watawala katika kujihakikishia kwamba wanapata ahueni ya kuendelea kubaki madarakani nyakati za chaguzi za kidemokrasia hapa Nchini.

Licha ya kwamba wapo watu wachache sana wanaoyafurahia matamko haya ya kupuuzwa yanayotolewa na baadhi tu ya wachumia tumbo wanaotimiza haja na matakwa ya mabosi wao, lakini pia ni dhahiri kwamba, wahusika wanayafanya haya ama kwa kujifanya wamesahau au kupuuzia kwa maksudi tu kiasi kwamba hawajui lengo kuu la wanyonge na walipa kodi wa Taifa hili ni kutaka ukombozi wa pili ili kuondokana na utawala huu dharimu wa CCM.

Kwa hiari yao wenyewe, wameamua kujivika umafia kwa kuwasaliti watanzania wanaodhurumiwa kila kukicha na Serikali hii inayodekezwa kwamba ni sikivu ya Chama legelege cha CCM.

Napenda kuwakumbusha kwamba, watanzania wa miaka hii ya Globalization na iliyojikita zaidi kidigital, sio wa enzi zile .
Watanzania wa sasa wanataka kuona kwa macho kile unachokifanya kwa niaba yao, huku wakipima misimamo yako ya utendaji kwa yale unayoyasimamia.

Chama hiki (Chadema) mnachokibeza leo kwa matamko ya kukaririshwa na kutolewa kafara kwa niaba ya watu fulani fulani wenye nia mbaya na Chadema kwa malengo yao binafsi, mnapaswa kushika adabu zenu kwa kuwaheshimu watanzania mamillioni kwa mamillioni waliokuwa wamekata tamaa ya maisha ndani ya Taifa lao.
Hiki mnachokifanya, sio siasa za kuwatia moyo wanyonge na ari ya kutafuta ukombozi wa pili utakaoweza kuwatoa gizani, bali ni kufanya mwendeleza wa siasa za majitaka ambazo hazitatukwamua kwa lolote kama wapinzani, isopokuwa tu kuendelea kuwakatisha tamaa watanzania wenye kiu na njaa ya mabadiliko ya kweli.

Wazungu husema, "If you can't convice them, you can confuse them", na napenda kuweka wazi jambo hili, endapo miongoni mwetu tutaendelea na tabia hii ya kutumiwa na vigogo wa Serikali hii ya CCM kwa manufaa yao, na tukakubali kuhubiri siasa za majitaka miongoni mwetu wenyewe hata pale pasipostahili kufanya hivyo, tutakuwa tunawapotosha wananchi baada ya kushindwa technic za kuwashawishi na kuwaelimisha ili wakubaliane na Sera, Falsafa, Ilani na Itikadi za Vyama/Taasisi zetu.

Mwisho kabisa, nikiwa kama Mwanachama mtiifu kabisa wa Chadema ninayeamini zaidi katika falsafa ya Chadema iitwayo "Nguvu ya Umma" The People's Power, nimalizie kwa kulaani vikali tena kwa nguvu zangu zote matamko yaliyowahi kutolewa, yanayoyolewa na yanayoendelea kutolewa na watu wachache waliofilisika kihoja baada ya kufukuzwa Chadema.

Pia kwa ya Wanachama, Wakereketwa na Wafuasi wa Chadema,nichukue fursa hii kuwapongeza kwa nia ya dhati kabisa viongozi wetu wa Chama ngazi ya Taifa ambao ni Mwenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa Mhe.Freeman Aikael Mbowe,
Katibu Mkuu wa Chama ngazi ya Taifa Dr.Willibroad Peter Slaa na Viongozi wote wa Mabaraza ya Chama ngazi ya Taifa kwa namna ya kipekeie wanavyofanya Kazi ya: Kukijenga na Kukiimaarisha Chama mpaka ngazi ya Msingi kwa Nchi nzima. Tumeanza na Mungu Tupo Na Mungu na Tutamaliza na Mungu. Mungu Ibariki Chadema