Close

Results 1 to 4 of 4
Like Tree2Likes
 • 2 Post By Masalu

Thread: JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI.

 1. #1
  Super Moderator Masalu's Avatar
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  1,095
  Rep Power
  10
  Likes Received
  76
  Likes Given
  41

  JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI.

  POLISI AKIJA KUKUKAMATA FANYA HIVI......

  Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
  o Muulize jina lake
  o Muulize namba yake ya uaskari
  Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.

  Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
  o Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.

  Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.

  Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
  Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe.

  Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa mtu anayetuhumiwa.

  Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale.

 2. #2
  Junior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  14
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI.

  Tanzania hayo mambo unayosema yapo kwenye vitabu vya sheria tu, mwananchi hana haki akikamatwa na ukitaka kusokomezwa jela au kubambikizwa kesi jaribu kujitia mjanja kuwaelezea haki zako, hapa mwenye haki mwenye pesa polisi na hata mahakamani.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  122
  Rep Power
  7
  Likes Received
  7
  Likes Given
  2

  Re: JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI.

  Asante mdau.
  Niliwahi kukamatwa na mamwela kisha wakanidai kitambulisho.
  Nikawapa cha mpiga kura.
  Ajabu na kweli, akadai eti hivi vitambulisho vya kura vingi ni feki?
  Nilimshangaa sana...........kama alishajua vingi ni feki, kwa nini watengenezaji hawakamatwi?
  au inteligensia ya polisi ipo kwenye kuzuia mikutano ya UKAWA tu?

 4. #4
  Junior Member
  Join Date
  Sep 2014
  Posts
  11
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI.

  Ukiwa legelege kweli utaonewa lkn ukikomaa kudai haki zako utazipata ndio tz ilivyo kaka!

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •