Close

Results 1 to 15 of 15
 1. #1
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Exclamation USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.  Najitokeza katika safu hizi za MF kuhitaji msaada katika hili;
  Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23,nilitokea kumpenda sana binti mmoja jina lake (....) naye akakubaliana nami ,tukapendana sana tena kwa dhati.Siku hadi siku shida na matatizo yake yote nilimtatulia.

  Basi akaona isiwe tatizo, akaniambia mimi nimekupenda sana na naona thamani na furaha kuishi nawe katika hii dunia na hata ahera hivyo naomba nikakutambulishe nyumbani kwa baba na mama na ndugu zangu wakufaham.

  Kwakua nilimpenda hata zaidi yake nikaona hii ni baraka na bahati ya pekee na wala nisikawie kukubali huenda akabadili mawazo.Nikamueleza basi jitahidi iwe ndani ya siku hizi mbili kwani huenda nikasafiri kikazi baada ya siku mbili zijazo.Kiukweli sikuwa na safari bali nilihitaji nisije nikachelewa akabadili mtazamo.

  Basi kama nilivyo mueleza akatekeleza na siku ya pili tukaenda kwao,baba na mama yake walifurahi kuniona pia na ndugu zake,.Baba akanieleza nashukuru kumuona binti yangu na kumpenda,jitahidi baada ya miaka miwili kumlea liwe jukumu lako, kwani wakati huo alikuwa akisoma chuo kimoja jijini Dar - Posta cha usimamizi wa fedha.

  Kwakuwa nilikuwa tayari nina kazi sikuona tatizo nikamueleza baba hili sitatizo kwangu na nimefurahi sana kusikia hivyo nakuahidi mimi nitampenda na kwamwe sitothubutu kumuacha na zaidi baba kwa miaka hii miwili iliyobaki mimi nitamsomesha.Baba na mama yake walifurahi sana kusikia hivyo.

  Basi sikukawia kuanza majukumu yangu,nilimsomesha na shida zake zote nilimtatulia tena kwa wakati.Muda wote huo hatujawahi kuingia katika mahusino ya kimapenzi kwani yeye alikuwa wadini nami vilevile.

  Leo amakweli najikuta nikitoa machozi kama mtoto,binti kamaliza chuo MUNGU kamsiidia nimemtafutia kazi na amepata.
  Sasa ananieleza "Mama yangu ameniambia mimi siwezi ishi na wewe,nami nimeona kweli huwezi ishi na mimi naomba utafute mchumba mwingine mimi tayari nina mchumba na wala sikutaki tena."


  Nilitamani dunia ipasuke niingie lakini...,kweli inaniuma,mimi fedha zote nilizo msomesha na kumsaidia sijali bali muda niliopoteza kumsubiri ndio kidonda ndugu kwangu huenda angenieleza mapema leo ningekuwa hata na mtoto mmoja.
  Kwa upande wa baba yake yeye binafsi anaonesha kutoafikiana na mtazamo wa binti na mamaye lakini ndio hana sauti mbele yao.

  Sifahamu hata tatizo ni nini ama kwakuwa nimesimamishwa kazi,sielewi,ama huyo aliye mpata ana hela sana sifaham,ama....
  nabaki na mtindio wa mawazo.....

  Wana MF naomba msaada wenu katika hili, kwani limechukua nafasi kubwa ya akili yangu na hata ufanisi wangu wa kazi umeathiriwa kwa kiasi kikubwa , wakati mwingine nafikia hatua ya kukata tamaa,lakini kamwe sito kata tamaa lakin sifahamu hata kama yatapita haya!!!!
  Msaada tafadhali.
  Last edited by MV Salama; 25-02-2014 at 04:17.

 2. #2
  Senior Member
  Join Date
  Dec 2013
  Posts
  123
  Rep Power
  7
  Likes Received
  3
  Likes Given
  0

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Utafanya makosa makubwa km utaacha hisia zako za kimapenzi zitawale maisha yako. Ni jambo la kumshukuru Mungu yametokea hayo kabla hujafunga naye ndoa, inawezekana Mungu amekuepusha na janga kubwa. Fikiria km mama anamtumia au anaungana na mwanae katika kutapeli wanaume, bila shaka hafai kuwa mkwe wa mtu mwenye heshima zake.

  Wala usilalamikie muda wako uliopoteza, hujapoteza kitu bali umepata nafasi ya kujifunza zaidi jinsi binaadamu walivyo na pengine kuanza sasa kuwa na tahadhari si kwenye mapenzi tu bali hata maisha yako yote kwa ujumla.
  MSHUKURU MUNGU AMEKUEPUSHA NA BALAA!

 3. #3
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Nashukuru sana Jididi, Mungu akubariki na nimejifunza jambo na somo kubwa kutoka kwako.
  Asante.

 4. #4
  Junior Member apakak's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  11
  Rep Power
  0
  Likes Received
  1
  Likes Given
  0

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Mkuu komaa tafuta hela achana na mawazo ya huyo mwanamke

 5. #5
  Junior Member
  Join Date
  Mar 2014
  Posts
  3
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  1

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  binti hakuwa na penzi la kweli kwako, ila alikuwa anatafuta kitu toka kwako.Nakushauri achana na mawazo juu yake kama ni muumini wa dini basi jaribu kufunga na kumwomba Mungu akusaulishe na hali hiyo na uweze kupata mke bora kwa maisha yako.Hili ni funzo uwe makini maana wanaume wengi wamesomesha mabinti, wakiwategemea wawe wake zao kumbe sio. Mbeleni wanawakimbia.

 6. #6
  Senior Member Kilaza's Avatar
  Join Date
  Feb 2014
  Posts
  3,033
  Rep Power
  10
  Likes Received
  8
  Likes Given
  0

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Quote Originally Posted by apakak View Post
  Mkuu komaa tafuta hela achana na mawazo ya huyo mwanamke
  nakuunga mkono.
  Mv Salama jiangalie wap umekosea na usirejee tena kosa km ilo achana na uyo mwanamke angalia maisha yako

 7. #7
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Hii vi vita kali.

  Click image for larger version. 

Name:	10247240_688747021193751_2768188109640413479_n.jpg 
Views:	552 
Size:	24.9 KB 
ID:	430

 8. #8
  Junior Member
  Join Date
  Oct 2014
  Posts
  3
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  0

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Pole sana mkuu, we kinachotakiwa ni kuangalia mbele sahau yote japo itachukua muda.
  What Goes around Comes around, huyo bint atakumbuka ishakua Too late.

  Sema naona watu tunatofautiana mie msimamo wangu siwezi kumsomesha mchumba hata kwa fimbo naweza kumsomesha mke wng au mama watoto hata akizingua atasaidia na watoto wetu

 9. #9
  Member
  Join Date
  Jul 2014
  Posts
  30
  Rep Power
  0
  Likes Received
  0
  Likes Given
  3

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Kaka u must control your emotion first..utafanikiwa

 10. #10
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  213
  Rep Power
  7
  Likes Received
  18
  Likes Given
  11

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  mkuu tunasomeshaga tulio wamimba tu tena baada ya kuzaa usirudie tena kosa hilo

 11. #11
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Mkuu Tanira tatizo lilikuwa imani hairuhusu..

  Shukrani sana kwa wote na yote kwani kwa sasa hali yake limeisha ni mbovu sana kwani yule bwana aliyemfanya anisaliti amempatia mimba kisha kamtelekeza na binti mwenyewe kazi alisha fukuzwa so let it be a special lesson kwa madada zetu wenye tabia ya usaliti.

  Alikuja na mamaye kuniomba radhi ati turudiane naye bali tayari ilishakuwa wasalimie kigoma ya kiba.

 12. #12
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Tafuta njuluku mwanangu achana na huyo maku.
  Last edited by KISIKI; 07-01-2016 at 16:44.

 13. #13
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Shukrani mkuu Kisiki..

  Nshapata. ...

  Ndio nikamwambia awasalimie kigoma Kisha awaambie nshaoa....

  Hahahahahh.... Kwakupindua maneno Hivi cyber crime haikupati....

 14. #14
  Senior Member MV Salama's Avatar
  Join Date
  Jan 2014
  Location
  New York
  Posts
  1,880
  Rep Power
  8
  Likes Received
  104
  Likes Given
  80

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Shukrani mkuu Kisiki..

  Nshapata. ...

  Ndio nikamwambia awasalimie kigoma Kisha awaambie nshaoa....

  Hahahahahh kwa mtindo huu wakupindua maandishi cyber crime haikupati mkuu...

 15. #15
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: USALITI HUU UNAUMIZA JAMANI.

  Mkuu MV Salama tafsida imezingatiwa.

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •