Nimefurahi kusikia nami ni miongoni mwa watanzania wachache waliopendekezwa kushiriki katika Changamoto muhimu ya katiba ya nchi yetu.

Natambua kuna maelfu ya watanzania wenye uwezo mkubwa na sifa za kutosha kunishinda ambao walistahili, lakini nafasi nimepewa mimi.

Nakishukuru chama changu kwa kulipendekeza jina langu TCD ambako nao waliliwasilisha Ikulu hadi kupelekea uteuzi huu muhimu.

Namshukuru Rais na Watanzania wote kwa kunipa fursa hii.

Jambo moja la msingi ni kuwa "NITAKWENDA KATIKA BUNGE LA KATIBA KUTUNGA KATIBA YA WATANZANIA NA SIYO YA CHAMA CHANGU",
Kila hoja nitakayoisimamia lazima iwe na mvumo wa "......watanzania wanataka hili liwemo".

Hofu yangu kubwa ni kuwa, ikiwa tutaruhusu misimamo ya Vyama katika Bunge hili, ni chama chenye wabunge wengi ndiyo kitatoa katiba, na makundi mengine yenye wabunge wachache na hoja za msingi, yatadharauliwa na hoja kutupwa mbali.

Mungu Ibariki Tanzania.