Jana majira ya saa moja jioni Makamu M/Kiti wa UTG Taifa, Bi.Eliza Ebeny na mwanae mchanga waliswekwa rumande kituo cha Polisi Oysterbay. Licha ya mtoto kuwa mgonjwa Polisi walikataa asipatiwe huduma. Tuliwasiliana na RPC lakini akasita kutoa ruhusa mtoto akatibiwe.

Majira ya saa 6 usiku mtoto akazidiwa akiwa kituoni. Polisi wakamchukua harakaharaka na kumpeleka hospitali Mwananyamala. Eliza alishauri wampeleke hospitali aliyokuwa akitibiwa maana kuna daktari bingwa wa watoto (pediatrician) aliyekua akimhudumia tangu mwanzo ambaye anafahamu vzr historia ya mtoto. Lakini polisi walikataa kwa hoja kwamba ni lazima atibiwe hospitali ya serikali.

Akashauri basi wampeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako ndipo alipojifungulia. Polisi wakakataa. Wakampeleka Mwananyamala kwa nguvu, ambapo alielekezwa kwa nesi ili ampe huduma. Eliza akasema kwa kuwa mwanae alikua akitibiwa na daktari bingwa, ni vigumu kwa nesi kuweza kumhudumia. Zaidi sana anaweza kumuongezea matatizo.

Akashauri kama ni lazima kuhudumiwa hospitali ya serikali basi waende Muhimbili ambapo kuna madaktari bingwa, na ndiko alikofanyiwa upasuaji. Lakini Polisi wakakataa. Kwa ubabe wakamrudisha kwenye gari na kumbwaga yeye na mwanae.

Hata hivyo hawakuondoa gari. Wakabaki hapo hadi saa 10 alfajiri akiwa chini ya ulinzi wa askari 7 wenye silaha (mithili ya jambazi). Kwa kuwa mtoto ni mchanga, na mama yake amefanyiwa upasuaji upepo na baridi vikaanza kuwaathiri.

Saa 9 usiku akapelekewa masweta kwa ajili yake na mtoto. Lakini polisi wapakataa asipewe. Kwahiyo wakapigwa baridi na mwanae kuanzia saa 6 usiku hadi saa 10 alfajiri bila kuwa na chochote cha kuwafunika. Kisha wakamrudisha kituoni Oysterbay bila mtoto kupatiwa huduma yoyote ya matibabu.

Asubuhi ya leo familia ya Eliza imekusanyika kituoni na kutoa shinikizo kubwa kwa polisi, na hivyo polisi kulazimika kumuachia kwa dhamana. Lakini wameshindwa kumwambia kosa lake. Kwenye hati ya mashtaka wameandika makosa ya mtandao. Walipoulizwa ni makosa gani hawajaweza kueleza. Baadae wakasema amecomment kwa Mange. Akawauliza comment gani, ya tarehe ngapi na inasemaje? Wakashindwa kujibu.!Click image for larger version. 

Name:	eliza.jpg 
Views:	328 
Size:	25.3 KB 
ID:	1704