Close

Results 1 to 4 of 4
 1. #1
  Senior Member
  Join Date
  Jan 2014
  Posts
  2,867
  Rep Power
  9
  Likes Received
  76
  Likes Given
  130

  Wazee wa CHADEMA Mkanyeni Godbless Lema

  Wadau, amani iwe kwenu.

  Kwenye magazeti ya leo, umenukuliwa ujumbe mfupi wa simu ulioandikwa na Familia ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Ujumbe huo unasomeka kama ifuatavyo;

  "Karibu Arusha. Tutakudhibiti kama Mashoga wanavyodhibitiwa Uarabuni"

  Kwa jicho la kawaida unaweza usione uzito wa maneno hayo. Ila kwa hakika hayapaswi si tu kuandikwa na Mheshimiwa Mbunge bali pia na Mtanzania yeyote. Sijajua alifikiria nini mpaka kuandika hivyo. Sijajua ni wangapi pia amewahi kuwadhibiti mithili ya wanavyodhibitiwa mashoga Uarbuni.

  Najiuliza sana, nini tafsiri ya mashoga kudhibitiwa kama wanavyodhibitiwa Urabuni? Sina haja ya kuhitaji ufafanuzi wowote katika hili kwa maana najua kuwa ni kitu kibaya.

  Nitoe tu ushauri wa bure kwa CHADEMA. Mdhibitini Godbless Lema. Anawaharibia.

  Niwaombe pia wazee wa CHADEMA hasa wale waliosajiliwa wakiwa wazee huru kutoka CCM, Lowasa, Sumaye, Ntagazwa nk pamoja na wale wazee asili wa CHADEMA, Baregu, Mtei, Ndesamburo, Safari na wengineo. Mna nafasi ya kuwakanya watoto wenu. Msipofanya hivyo, kuna mwingine atachukua majukumu yenu.

 2. #2
  Senior Member KISIKI's Avatar
  Join Date
  May 2014
  Posts
  2,831
  Rep Power
  8
  Likes Received
  171
  Likes Given
  339

  Re: Wazee wa CHADEMA Mkanyeni Godbless Lema

  Na wazee wa ccm mkanyeni yule kijana wenu wa kiume tena kiongozi aliyeolewa kule Mombasa.

 3. #3
  Senior Member
  Join Date
  Aug 2014
  Posts
  2,379
  Rep Power
  8
  Likes Received
  144
  Likes Given
  164

  Re: Wazee wa CHADEMA Mkanyeni Godbless Lema

  Napenda watu jasili aina ya Lema.Mtu anayeleta za kuleta naye anastahili kupewa za kupewa.Arusha ni ya wana Arusha wenyewe .Na wenye Arusha wamemchaguwa Lema awaongoze,wewe wa kuletwa unapovimbishiana msuli na mwenye mji ni “uzwazwa” wa madaraka,ujumbe huo ni ujumbe sahihi.
  Last edited by Nyaluhala; 02-11-2016 at 14:14.

 4. #4
  Senior Member
  Join Date
  Jun 2015
  Posts
  722
  Rep Power
  5
  Likes Received
  23
  Likes Given
  1

  Re: Wazee wa CHADEMA Mkanyeni Godbless Lema

  kama ilvyo ada kwa CCM kuwa chachawangwe viongozi wa upinzani anao onesha kupingana na vitendo vya kifisadi ole wenu siku mtakayo ona nchi hii haikariki pale mtakapo chokoza eneo hilo mungu anwale mahala pepeoni Mawazo,amina Chifupa,Salome mbatia Deo filikunjombe Edward Moringe Sokoine na viongozi wengine wazarendo walio tangulia mbele ya haki
  punda hajasoma lakini kazi hakosi

Posting Permissions

 • You may not post new threads
 • You may not post replies
 • You may not post attachments
 • You may not edit your posts
 •