TATIZO LA MDORORO WA MABENK NCHINI Mtakumbuka zimekuwepo rumours, mijadala kuhusu mienendo ya Taasisi za kifedha kuyumba kukihusishwa na madai ya mdololo wa kiuchumi nchini...Jambo ambalo sio kweli....

Tanzania kwa sasa tuna mabeki 50 ambayo yapo chini ya usimamizi wa Benki kuu BOT.....zipo sababu kadhaa ambazo zinaweza au zimechangia kutisikika kwa mabenki nchini....

1. Kuboreshwa kwa Teknolojia ya mitandao ya Simu ambayo imeanza kufanya shughuli za kibenki Vijijini kumepelekea wananchi zaidi milioni 20 kati ya milioni 29 wenye laini za Simu kuhifadhi na kufanya miamala yao kupitia Simu zao za mikononi kitendo hicho kinafanya wananchi wengi kuhama kutoka kwenye mabenki kwenda kwenye Tigo pesa, m.pesa, eartel money, Ezzy pesa. Haloo Pesa......

2. Mitandao ya Simu kuanza kutoa mikopo ya kifedha kwa wananchi mfano M. Mpawa n.k hivyo kupunguza idadi kubwa ya wateja wa mabenki kwenda kukopa kwenye mabenki na kuhifadhi fedha zao benki...........

3. Kuongezeka kwa microfinance, vikoba, saccoss vikundi vya kufa na kuzikana vyote hivi vimefanya wananchi fedha zao nyingi kuzihifadhi huko na kukopa na kukopeshana kupitia huko jambo ambalo linaathiri na kupunguza idadi ya wateja wa mabenki..........

4. Riba kubwa 20% - 30% inayotozwa na mabenki nchini imechangia kwa kiasi kikubwa kukimbiza wateja wa mabenki na wateja wa mabenki wengine kushindwa kurudisha mikopo kwa sababu za ukubwa wa riba kwenye mikopo yao. Hivyo mabenki yanajikuta katika hasara kubwa...........

5. Kupungua kwa fedha ya anasa ambayo zimethibitiwa na serikali kwa kuipunguza kwenye mzunguko wa matumizi yasiyo sahihi kunaweza kuathiri uzalishaji au utoaji wa huduma kwa wateja waliochukua mikopo kwenye benki kushindwa kurudisha au kuchelewa iwe mikopo ya muda mfupi au muda wa kati au mrefu.....kama ililikuwa na mfungamano huo wa fedha za Anasa zilizofutwa na serikali ya Hapa Kazi Tu................

6. Ni ukweli usiopingika kuwa uamuzi wa serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima, kudhibiti suala la rushwa, kusimamia ulipaji wa kodi kwa wananchi wanastahili kulipa kodi, serikali kuamua kutumia machine za EFD katika kukusanya kodi.......

Ni ukweli usiopingika kuwa baadhi ya sekta zimeathirika na wafanyabiashara ambao hawakuzoea kulipa kodi katika biashara yao hivyo kupata faida Mara mbili..hivyo kama serikali inawabana kulipa kodi hawa wafanyabiashara ambao hawakuzoea kulipa kodi lazima washindwe kurudisha mikopo katika mabenki yetu..

Serikali inapokusanya wastani wa kodi ya Trilioni 1.1 kwa mwezi ukilinganisha na makusanyo ya billioni 850 kwa mwezi mwaka jana. Unaposikia mizigo imepungua bandarini lakini makusanyo ya kodi bandarini imeongezeka kwa akili ya kawaida itashangaa lakini ndio huo na hayo ndio yamewafanya watu hasa wafanyabiashara kujiondoa na kushindwa kurudisha mikopo ya mabenki automatic na sekta zinye mfungamano na hawa lazima ziathirike...

kama ungekuwa mtikisiko wa kiuchumi tungeona mtikisiko huo kupitia a) mfumuko wa bei (,inflation) lkn bado upo chini ya single digit.. B) thamani ya shilling yetu kwa dola (Value of Money) mwaka mzima sasa na zaidi dola moja imebaki na wastani wa shilling 2100 za kitanzania. C) viwango vya mishahara havijapungua au kuathiriwa na mfumuko wa bei au thamani ya shilingi ndani ya mwaka Mzima..........

Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa wastani wa asilimia 7.0 malengo ya serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mh Rais John Magufuli ni kuhakikisha uchumi wetu unakuwa kwa wastani wa asilimia 7.2.....

Hivyo ripoti ya benki kuu ya robo pili mwaka huu pato la Taifa limeendelea kukua kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na asilimia 5.8 ya robo ya pili ya mwaka jana. Pato hili la Taifa limefikia jumla ya Thamani ya trilioni 11.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 10.9 katika kipindi hicho mwaka jana.......
Huku shughuli zilizochangia ukuaji wa uchumi wetu kwa kiasi kikubwa zikiwa ni Uchukuzi, hifadhi ya mizigo, ujenzi, kilimo.n.k.........

imeonesha uimara wa uchumi wetu kukiwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni zinazofikia dola bilioni 4. Huku serikali ikiendelea kutumia fedha zake za ndani kuendesha shughuli za nchi............

Kipimo kikuu cha upimaji ukuaji wa uchumi huwa ni Pato la Taifa (GDP), Nguvu ya pesa ya nchi (value of money), akiba ya fedha za kigeni ndani ya nchi, mfumoko wa bei (inflation rate) n.k....

japo wananchi wengi huwa wanachanganya kati ya Ukuaji wa uchumi (Economic Growth) na Maendeleo ya kichumi (Economic Development)......

Kwa upande wa maendeleo ya kiuchumi kipimo kikuu huwa ni kipato cha mtu mmoja mmoja ikiambatana na hali ya maisha (living standard of life)
Mfano nchi ya Marekani ndio nchi inayongoza kwa ukuaji wa uchumi na uchumi imara lakini ukiangalia living standard ya watu wake hailingani na wananchi wa nchi za kiarabu au united Arab Emirates (U.A.E ) living standard ya maisha ya hawa watu ni nzuri sana mfano marekani tatizo la ajira ni asilimia 6.2 wakati nchi United Arab Emirates tatizo la ajira ni asilimia 0.3 inabidi wafanyakazi wa shughuli ngumu waagizwe huku Afrika na India wafanyakazi wa ndani, walinzi, madereva. N.k.

Mfano wa pili Nigeria ndio nchi inayoongoza kiuchumi barani Africa ikifuatiwa na Afrika kusini lakini living standard ya maisha ya wananchi wake hailingani na living standard ya maisha ya watu wa Libya ya Gadafi, au watu wa Rwanda, watu wa Morocco pamoja na kuwa uchumi wao umezidiwa na hizo nchi.........

Ushauri wangu kwa Benki za Tanzania

Ningekuwa mbunge ningepeleka hoja binafsi bungeni ya kutungwa kwa sheria ya matumizi ya fedha nchini kutoka katika mfumo wa cash system kwenda mfumo wa credit system ili kuyaokoa mabenki nchini. Kama ifuatavyo....

1. Sheria hii ingesaidia wananchi wengi kufungua account benki kwa ajili ya manunuzi, malipo au kupitishia fedha zao hivyo kuongeza wateja wapya nchi Nzima.......

2. Sheria ingetamka wazi kuwa manunuzi au malipo yoyote yanayoanzia milioni 2 na kuendelea lazima yafanyikie kupitia benki katika mfumo wa credit system kitendo ambacho sio tu kingeongeza wateja wengi wapya pia watu wangehifadhi fedha zao benki sio majumbani.....

3. Sheria hii ingesaidia kuongeza mapato ya serikali yanayopotea bure kwa sababu ya kutokuwepo mfumo mzuri mfano mtu anapangisha nyumba Nzima kwa mwaka milioni 12 serikali haipati hata shilingi kumi wakati sheria ipo wazi asilimia 12 ya kodi inapaswa kulipwa serikalini......Hivyo kodi ya Nyumba au pango ingelipwa kupitia benki na nakala ya mkataba wa Mpangaji na mpangishwaji copy moja sheria ingetamka ibaki serikali ya mtaa au kijiji kwa ajili ya kumbukumbu......

4. Sheria hii ingesaidia kupunguza fedha nyingi ambazo zipo mikononi mwa wananchi na kuzirudisha katika mabenki. Mh Rais Magufuli aliposema kuna fedha nyingi zipo mikononi mwa wananchi na hazipo kwenye mzunguko rasmi watu wengi hawakuelewa hadi leo....

Ukweli ni kwamba kupitia benki kuu kujua fedha ambazo zipo kwenye mzunguko na mikononi mwa watu ni jambo rahisi sana......

Lakini ni ushahidi uliowazi mwananchi wanatembea na fedha kwenye magari mtu anaenda kununua Nyumba, kiwanja, Gari milioni 100-300 fedha anatoa kwenye begi, gari, mfuko wa Rambo hii ni hatari sana serikali iatakosa mapato na benki zitakosa wateja........

5. Hizi benki zikae na benki kuu ziangalie namna ya kupunguza ukubwa wa riba. Maana riba ya 20%-35 mwananchi maskini hatoboi mtamfirisi au kuuza dhamana zake akishindwa kurrejesha mkopo wenu. Hivyo lazima benki ziwe rafiki kwa wananchi wa kawaida, wajasiriamali, wafanyabiashara n.k wasiozione benki kama kituo cha polisi kwa sababu ya ukubwa wa riba.......

6. Hivyo sheria hii itasaidia kuongeza idadi kubwa ya wateja wengi wapya na mabenki yatafungua matawi ya mabenki kila wilaya nchi Nzima. Pia benki zitapata akiba yingi ya fedha baada ya wananchi kulazimika kisheria kutumia mfumo wa credit system watu watahifadhi fedha benki kutoka mikononi kwa ajili ya kufanya malipo au manunuzi.... Pia serikali ya mh John Magufuli itapata kodi take....

Na Fahami Matsawili